Tunashukuru sana kwa michango yenu woteNakubaliana na wewe asilimia 100. Upo sahihi kabisa na ndivyo hali ilivyo. Ndiyo hali ninayopigana nayo. Soma ripoti yangu ya mwaka niliyotoa Aprili 2009 Bungeni.
Nimekuwa nikipigana wabunge wasiwe wajumbe wa Bodi za Mashirika haya ili kupunguza 'kugawana' misosi.
Nimepigania sana kuanzishwa kwa Office of State Entreprises ili kudhibiti mashirika na bodi zao. Au kuimarisha ofisi ya Treasury registrar.
Nimepigania Bodi kupewa mikataba ili kuwadhibiti.
Hawa wnasiasa wote wa CCM hawa mnaowasikia wanapiga kelele wamo kwenye mabodi au marafiki zao wamo kwa mabodi na wananipiga vita kwa kuwapinga. Lakini sitaacha maana ninaamini ni njia sahihi.
Nakubali mawaziri wanatumia vibaya mashirika yao, mawaziri wote kabisa na ninagombana nao sana. The other day i invoked act no. 3 to detain Mary Nagu and she ran from Dodoma and by the time parliamentary officer found her in Dar she had rectified what she did for NDC. I was to do the same to Ngeleja for not appointing TPDC Board for two years!
Nakubaliana na wewe kabisa na ndio maana nasema sisi wanasiasa tufanye oversight (our constitutional role). Wataalamu wafanye kazi zao. Lakini sisi tunawapowaingilia katika kazi zao ndio tunaharibu. Thats my stand kaka!
Hii NOOR OIL ilikuwa imekuja kwa gear ya kujenga pipeline kuanzia Dar mpaka mwanza na kujenga refinery in Dar. Hii ndiyo ilikuwa gear yao. Lakini ofisi zao zilikuwa Water Front (Former Nasaco Building) na MD wake ni dada mmoja, I think wa kiarabu au kihindi halafu inasadikika ni dadake/nduguye RA na ni mke wa mheshimiwa sana. Sasa kama ndivyo ilivyo then......wale wenye data tuanikieni kila kitu ili tujue mapema na tupige mbiu mapema kabisaaa!!!!Kwa kuongezea, kwa nini serikali imeingia kwenye mikataba na IPTL, RICHMOND etc. kwa mfano pesa za richmond za mkataba $172million ( three years contract) zingeweza kununua mitambo mipya 3 ya 100MW toka GE/ROLL ROYCE/ DRESSALAND/SIEMENS etc. bahati nzuri nafanya kazi kati ya hizo kampuni hapa Ohio, gharama ya mtambo (equipment only ya 100 MW ni 30-35million) ukiongeza installation cost , shipping etc ambayo ni 25-75% ya cost ya equipment. utaona kwamba mtambo mmoja ni kati ya 50-60 million mpaka kuwashwa. juzi juzi tu Tanesco wametangaza tender ya 100MW kwa gharama ya $120million, hizi pesa zingetosha kununua mitambo 2 ya 100MW. miezi kama miwili niliongea na classmate wangu tuliyekuwa naye Colombia university ambaye anafanya kazi roll-royce internation kaniambia kuna jamaa wanaitwa noor oil ya waharabu na wahindi wamepeleka bid ya hiyo tender kwa kutumia jina la roll royce kwa haraka haraka nikamwambia huyo classmate wangu kwamba mbona hawa jamaa ni wale wa richmond wanakuja kwa sura nyingine, kwa hiyo tunasubiri tender itoke kwa kweli safari hii tutatumia international lawyer kuwafikisha hawa noor na tanesco kwenye international court ya corruption. haiwezekani mtambo wa 100mw ambao gharama yake ni 50-60million wanunue kwa 120million.
Unachotakiwa kutambua ni kuwa TANESCO, kwa kufuata sheria, walikuwa na muda wa kutosha kuanza mchakato wa kunua mitambo mipya mapema. Hukukuwa na haja ya kuchapia au kuvizia mitambo chakavu katika hilo.
Maamuzi ya kununua mitambo hayapaswi kushabihiana na maamuzi ya kunua maandazi au kanga; kwamba ukiwa na pesa mfukoni basi unakwenda kununua utakacho mara moja.
Katika hili la kupendekeza TANESCO inunue mitambo chakavu ya Dowans, Zito Kabwe ama hakuwa na vision au kulikuwa na msukumo kutoka nje ya 'uwezo' wake. Hakuwa Zito tunayemjua.
Ndio wasomi wetu sasa wakiondolewa nchi itaendeshwa na naniPiga chini Waziri na uongozi wote wa Tanesco..........damn!
Kama Richmond ina uhusiano na RA then impliedly NOIT nayo ina uhusiano. Kumbuka MD wake hapa TZ ni dada yake ambaye pia inasadikika anauhusiano wa kimapenzi au wa mke na mume mheshimiwa mkubwa saana. Hii pia ni prompt nyingine ya kuiangalia.Richmond ndugu yangu hawamo. Huyu mwandishi alichanganya tu. Wao ndio walipewa mwaka 2004 wakashindwa.NOIT sasa ni Qatarians, Russians and CCM!
Thanks alot for very prompt responses and your sources backing your arguments. Impressed!
Then I think the general public was mislead through the media and even the Mwakyembe report as it was portraying as the whole was actually spent. Most of us has had that notion in our minds which was wrong.Shukran kwa maelezo mazuri sana. Tender ya TANESCO ilitangazwa katika magazeti ya kimataifa kwa kampuni zinazojenga mitambo na sio middlemen. Hivyo hao NOIT hata wafanyeje hawawezi kupata. Sasa na wewe nawe kwa nini hukushauri kampuni unayofanyia kazi ibid?
TANESCO hawakutangaza bei ya kununua. Wao walisema wanataka mtambo mmoja wa 100MW na mwingine 60MW. Bei itatokana na wazabuni waliomba, atakaetoa bei nzuri na mtambo imara ndie anapaswa kupata. Bei bado na sio taratibu za tenda kusema ninanunua kwa bei hii, sasa zabuni haitakuwa na maana.
Hebu niambie, katika hiyo kampuni yako inachukua muda gani kuanzia order mpaka commissioning?
Mwisho - umezungumzia fedha za Richmond zingeweza kununua mitambo kadhaa. Lakini hatukulipa hizi fedha kwa Richmond. Tuliwapa advance ya 30m usd halafu tukakatana katika charges. Mpaka mkataba wa Dowans unavunjwa tulikuwa tunawadai 8m usd zilizobaki.
Kama katika vitambulisho - serikali haikai na 172m usd na kusema mkataba huu pesa hizi, hapana. Serikali haina pesa zilizokaa kwa kuchotwa. Huwa zinalipwa kidogokidogo kutokana na makusanyo ya kodi, Hivyo mkataba wa Richmond ulikuwa umesambazwa over 2 years na zile 172m usd zilikuwa zilipwe over 2 years kutokana na kiwango cha umeme tulichokuwa tunanunua. Nadhani umenielewa!