Sikia mkuu, hizo ulizosikia ni uchimbaji mpya wa visima vipya. Mnazibay, Msimbati, songosongo tayari kuna visima vya Gesi na hatua hiyo imeshapita, Dangote anauziwa Gesi na anazalisha umeme wake mwenyewe kupitia hiyo gesi. Gesi itauzwa majumbani, na viwandani lkn pia itatumika kama chanzo cha umeme wa uhakika. Umefikiria 70T kwa maono mafupi, mradi wowote lazima uwe na payback period, na hapo unapimwa kwa short term, medium, au Long term na kwa investment hiyo ujue ni Long term yaan kuanzia miaka 10 na kuendelea, umeme wa uhakika utaleta vichocheo halisi vya uchumi kama viwanda nk hivyo kupelekea pato kubwa la nchi na TANESCO hata kuweza kulipa hilo deni.