saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Kuna ndugu yangu alifika kununua godoro kwa wakala wa kampuni kongwe inayotengeneza magodoro ya TanFoam. Wakala mwenyewe anaitwa Yahaya Mono Msuya yuko Arusha mjini mtaa wa mjini kati karibu na soko kuu, yeye alitaka kununua godoro la Tanfoam badala yake walimshawishi kununua godoro la Besti wakidai nalo linatengenezwa na TanFoam.
Baada ya ushawishi wa muda na kutumia jina la TanFoam huyu ndugu yangu alikubali kulinunua godoro la futi 4 x6 unene inchi 8 kwa Tshs 250,000/= ila kwenye risiti walimwandikia 150,000/ kukwepa kodi ya Serikali. Baada ya kuanza kulitumia godoro lenyewe ni sawa na yale mengine yanayobonyea wala halifanani na TanFoam.
Ndipo alianza kufuatilia ktk maduka mengine na kukuta linauzwa kati ya Tshs 150,000/ na 170,000/ na ndipo alipogundua ametapeliwa na kuibiwa na hawa mawakala.
Baada ya kurudi kwa wakala tajwa hapo juu kuwaeleza ukweli walimkatalia kumrudishia hela yake waliyojipatia kwa njia ya udanganyifu na uwizi wa kuaminika.
Tunawaomba TanFoam kama inawezekana wawe wanatoa bei elekezi na kutueleza km kweli magodoro ya Besti ni ya kwao.
Serikali iwafuatilie hawa mawakala matapeli na wanaokwepa kodi stahiki ya Serikali. Huyu ndg yangu nimemshauri aende kwenye vyombo vya dola ikiwemo Jeshi la Polisi na TAKUKURU.