Pre GE2025 Tanga: Bodaboda wamchangia Rais Samia Tsh Milioni 1 kwa ajili ya kuchukua fomu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Sijajua tuko season au episode ya ngapi lakini ile tamthiliya yetu ya kuelekea uchaguzi mkuu inaendelea

=====================

boda-pic.jpg

Wanachama wa Umoja wa Wamiliki wa Waendesha Pikipiki na Bajaji Wilaya ya Tanga (Uwapibata) wamechanga Sh1 milioni kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais kwa mwaka 2025.

Fedha hizo wamezikabidhi leo Januari 4, 2025, wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, jijini hapa.

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo, Mwenyekiti wa Uwapibata, Mohamed Chande amesema lengo la kumchangia Rais kuchukua fomu ni baada ya kuwawezesha kupata mikopo ya asilimia 10 na kushusha faini kutoka Sh30, 000 hadi Sh10,000.

"Sisi bodaboda na bajaji kwa umoja wetu tumeamua kuchanga fedha hizi lengo ni kumtia moyo Rais Samia sababu kwa mapenzi yake ameamua kututhamini na ametubadilisha jina kutoka bodaboda na kuwa maafisa usafirishaji," amesema Chande.

Madereva hao pia wamemwomba Mbunge wao, Mwalimu, kuwatunishia mfuko wao wa kukopeshana ili wapate leseni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwalimu amesema alishakutana na viongozi wa Uwapibata nyumbani kwake mara mbili hivi ambapo walijadili changamoto zao.

Katika utatuzi wa changamoto hizo, amesema amewashirikisha wadau ili kupata fedha za kujenga vituo vya bodaboda ambavyo vitakuwa kitega uchumi na atahakikisha anaweka intaneti.

"Ndoto yangu nataka kuacha alama ya kujenga vituo vya bodaboda katika mitaa yote 181 iliyopo jijini Tanga na nihakikisha naviweka katika mfumo wa satelite ili wateja hata wakiwataka wanapiga simu tu," amesema.

Kuhusu changamoto wa mfuko wao, Mwalimu ametoa Sh10 milioni kwa ajili ya bodaboda zaidi ya 1,000 kupata leseni za udereva ili waache kukimbizana na askari polisi, huku pia akiwawekea lita mbili mbili za mafuta katika bodaboda na bajaji 500 za jijini Tanga.

CHANZO: MCL

Lucas Mwashambwa ChoiceVariable Tlaatlaah lini mtatolea mama yenu hela ya fomu ya kugombea?
 
Igizo, yaani boda boda na bukubuku zao za mbinde juani huku wakikoswakoswa na malori rodini eti wachange milioni 1 kwa ajili form ya Samia??
Hivi Ummy anatuonaje watz?!.
 
Hata mimi muda ukifika ni lazima nimchangie Mama yangu Mpendwa na kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Rais Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan pesa ya kuchukulia Fomu ya Urais.

Ila kwa sasa ninaendelea na kazi ya kumtafutia kura kila uchao. nafanya kazi ya kuwaeleza mambo makubwa na mazuri ambayo Mama yetu ameyafanya.ambapo hata wao wanakiri kuyaona na yanawagusa moja kwa moja na yamebadilisha Maisha yao na kuleta matumaini na tabasamu katika nyuso na mioyo yao.
 
Wakuu,

Sijajua tuko season au episode ya ngapi lakini ile tamthiliya yetu ya kuelekea uchaguzi mkuu inaendelea

=====================

Fedha hizo wamezikabidhi leo Januari 4, 2025, wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, jijini hapa.

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo, Mwenyekiti wa Uwapibata, Mohamed Chande amesema lengo la kumchangia Rais kuchukua fomu ni baada ya kuwawezesha kupata mikopo ya asilimia 10 na kushusha faini kutoka Sh30, 000 hadi Sh10,000.

Lucas Mwashambwa ChoiceVariable Tlaatlaah lini mtatolea mama yenu hela ya fomu ya kugombea?

View attachment 3192402
Gentleman,
Fursa na nafasi kwa family na members wote JF kufanya hivyo bado iko wazi pia. Msiogope hata kama ni kidogo itapokelewa .

ni muhimu kujitolea bila kujibakiza kwenye jambo muhimu la kizalondo kama hilo na bilashaka utakua umechangia jitihada za kuiunganisha taifa na kuifungua nchi.

Changia kadiri uwezavyo,
ili kumpa nguvu na moyo mama huyu kiongozi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, ili apate nafasi nyingine ya kikatiba kuendelea kuiongoza nchi na taifa letu, kuelekea maendeleo endelevu kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa maslahi mapana ya taifa letu,🐒
 
Wakuu,

Sijajua tuko season au episode ya ngapi lakini ile tamthiliya yetu ya kuelekea uchaguzi mkuu inaendelea

=====================

View attachment 3192407

Wanachama wa Umoja wa Wamiliki wa Waendesha Pikipiki na Bajaji Wilaya ya Tanga (Uwapibata) wamechanga Sh1 milioni kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais kwa mwaka 2025.

Fedha hizo wamezikabidhi leo Januari 4, 2025, wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, jijini hapa.

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo, Mwenyekiti wa Uwapibata, Mohamed Chande amesema lengo la kumchangia Rais kuchukua fomu ni baada ya kuwawezesha kupata mikopo ya asilimia 10 na kushusha faini kutoka Sh30, 000 hadi Sh10,000.

"Sisi bodaboda na bajaji kwa umoja wetu tumeamua kuchanga fedha hizi lengo ni kumtia moyo Rais Samia sababu kwa mapenzi yake ameamua kututhamini na ametubadilisha jina kutoka bodaboda na kuwa maafisa usafirishaji," amesema Chande.

Madereva hao pia wamemwomba Mbunge wao, Mwalimu, kuwatunishia mfuko wao wa kukopeshana ili wapate leseni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwalimu amesema alishakutana na viongozi wa Uwapibata nyumbani kwake mara mbili hivi ambapo walijadili changamoto zao.

Katika utatuzi wa changamoto hizo, amesema amewashirikisha wadau ili kupata fedha za kujenga vituo vya bodaboda ambavyo vitakuwa kitega uchumi na atahakikisha anaweka intaneti.

"Ndoto yangu nataka kuacha alama ya kujenga vituo vya bodaboda katika mitaa yote 181 iliyopo jijini Tanga na nihakikisha naviweka katika mfumo wa satelite ili wateja hata wakiwataka wanapiga simu tu," amesema.

Kuhusu changamoto wa mfuko wao, Mwalimu ametoa Sh10 milioni kwa ajili ya bodaboda zaidi ya 1,000 kupata leseni za udereva ili waache kukimbizana na askari polisi, huku pia akiwawekea lita mbili mbili za mafuta katika bodaboda na bajaji 500 za jijini Tanga.

CHANZO: MCL

Lucas Mwashambwa ChoiceVariable Tlaatlaah lini mtatolea mama yenu hela ya fomu ya kugombea?
Kwishaa Tanga ukichangiwa umekwishaa
 
Back
Top Bottom