Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. GETERE - TANGA CEMENT INA HIFADHI YA MALIGHAFI YA SARUJI HUKU TWIGA CEMENT WANA MITAMBO MIZURI YA KUZALISHA SARUJI
Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini Mhe. Boniphace Mwita Getere amegusia suala la Twiga Cement na Tanga Cement huku akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakati wa kusomwa kwa bajeti ya Wizara na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
"Ni lazima serikali iwaangalie watu wa Tanga wananung'unika nini? hili jambo (la Twiga Cement kutaka kuinunua Tanga Cement) lisichukuliwe kama kawaida. Ni kweli mtu anayemiliki kiwanda (Tanga Cement) hana uwezo? " Mwita Getere, mbunge wa jimbo la Bunda vijijini.
"Kiwanda cha Tanga kina hifadhi kubwa ya malighafi ya kuzalisha saruji (clinker) halafu kiwanda cha Twiga Cement kuna mitambo mizuri ya kuzalisha saruji, sasa hapa utapima mwenyewe je ni kitu gani kitahama endapo Twiga Cement itainunua Tanga Cement? Je ni clinker itahama kwenda Dar es Salaam au mitambo itahama kutoa Dar es Salaam kwenda Tanga?" Mwita Getere, mbunge wa jimbo la Bunda vijijini.