Tanga kiingilio elfu 20! Hawa TFF wako sawa sawa kweli?

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Kuna watu kweli akili zao sijui kama Zina weza kufikiria vyema hasa katika kipindi hiki kigumu na Cha mpito

Tanga wameangalia mechi 2 mfululizo kwa KIINGILIO Cha elfu 10 na kuendelea .tena ndani ya siku tatu mtu atoe tena elfu 20 ili kuona fainali?

Au Azam wamewaambia muweke viingilio vikubwa ili watu wasije walipie ving'amuzi?

Acheni hizo habari aiseeee ! Punguzeni viingilio hivyo

Sijawai ona ngao ya jamiii hata moja nchin ikawa na KIINGILIO kuanzia elfu 20

Maisha ni magumu sio mchezo
Kwanza Tanga yenyewe kavu kinoma
Kila mtu anadaiwa vicoba sio mume sio mke

Punguzeni viingilio acheni kupima watu kama wanapenda Mpira au hawapendi

Majukwaa mtayakuta meupe hayo .watu wanawaangalia tu.

Mtachagua Moja wenyewe either kuingiza watu Bure kama yanga Africa au kupunguza KIINGILIO.

Yangu ni hayo na nimekaaa pale naangalia uwanja utakavyokuwa mweupe.
 
Walikuwa wanadai wanapeleka game kama hizo huko ili wenyeji wapate kuona live mechi kubwa ila cha ajabu kiingilio kinawatarget watu waliotoka Dar huku wenyeji wakibaki kuangalia mchezo kwenye TV.

Pia ukijumuisha gharama za timu zote kuanzia usafiri na malazi zinazidi mapato yote yaliyopatikana. Kama lengo ni mapato kuchangia jamii ni afadhali timu zingetuma cash money zipelekwe kwa wahitaji.
 
Kuna watu kweli akili zao sijui kama Zina weza kufikiria vyema hasa katika kipindi hiki kigumu na Cha mpito

Tanga wameangalia mechi 2 mfululizo kwa KIINGILIO Cha elfu 10 na kuendelea .tena ndani ya siku tatu mtu atoe tena elfu 20 ili kuona fainal...
Hii ilikuwa planned before. Ndio maana waliforce sana Simba na Yanga zikutane
 
Hiki kiingilio hapana aisee, kwa maisha yetu sidhani kama ni kiingilio sahihi.
 
Wanazingua sana hawa, hapo wanadai wanafanya hivyo makusudi ili kupunguza idadi ya watu uwanjani.
 
Ni sawa kabisa kwa principle ya demand na supply,ukiweka 10 elfu itakuwa shida
Factors that affect demand. 1. Consumers Income. Kumbuka demand ni willing and ability, unaweza ukawa na willing but hauna ability, unaweza ukawa na ability ya kununua maji ya kilimanjaro ila ukaamua kununua afya.

Kipato cha jamii husika eneo hilo kitaathiri hiyo demand, watu wapo willing ila hawana uwezo.
 
Tuweke mkazo kwenye utafutaji wa hela elfu 20 ni dola 8 tu wenzetu kiingilio cha mechi ndogo kabisa Dola 25
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…