Tanga Mjini ni pagumu sana aisee

Njoo Zanzibar, maeneo ya Shamba, Bwejuu, Matemwe ujenzi wa Mahoteli makubwa unaendelea
 
Dah umenikumbusha mbali sana mkuu wakat nimemaliza chuo nilivamia Hilo jiji kutafuta ahueni ya maisha dar niliona ya moto sana,..niliondoka dar na begi langu na nguo mbili tu,..
Nikafkia maneno flani ivi wanapaita makorora Kwa mwanngu Mmoja naye anachumba kimoja ana ish na mkewe na watoto watatu sio poa Yan..
To make story short nilienda kujichanganya kwenye soko la makorora pale kutafuta chchte ule mji n ngumu sana aisee ,hela ni ngumu sana kuikamata,unakuta sokon pale mfanyabiashara mwenye mtaji mkubwa ana laki anaizungusha..
Viwandani uko nimezunguka sana ule mkoa golf yote Ile nikimaliza,..vingi vimeshajifia na vilivyobaki vinapumulia machine hakuna kazi..
Aisee nilipambana nilivoshka elfu hamsini nikarudi town tu.
 
Afadhali hata Singida unaweza ukasikia honi za magari.
 

Tanga sijawahi paelewa, kutoka Kilimanjaro /Arusha ukaenda Tanga, utapashangaa, yapo slow, mavivu, story, malengo Mjini Kabisa ni magofu hayana watu! Ajabu sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…