Tunazidi kulisogelea jambo letu 2025, tushiriki kwa umoja wetu katika uchaguzi wa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 kuhakikisha tunapata viongozi bora.
Your browser is not able to display this video.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Michael Kaniki Kaimu Afisa ushirikishwaji Jamii Mkoa wa Tanga amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kujiepusha na uvunjivu wa amani wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025.
ASP Kaniki ameeleza hayo wakati akizungumza na Wananchi kupitia kituo cha Radio cha TK FM kilichopo Jijini Tanga katika kipindi chake cha Amka na Tk na kushauri wananchi kuhakikisha jambo la kutunza amani linakuwa ni kipaumbele kwao.
Amesema kuelekea kwenye chaguzi kuna kuwa na matukio mbalimbali ya ushawishi, hivyo makundi yote yanatakiwa kusimama na kauli moja ya kulinda, huku michakato mingine ya uchaguzi ikiendelea.