Pre GE2025 Tanga: REA inatekeleza miradi minne ya kusambaza umeme kwa thamani ya shilingi bilioni 137.87.

Pre GE2025 Tanga: REA inatekeleza miradi minne ya kusambaza umeme kwa thamani ya shilingi bilioni 137.87.

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage amesema kuwa Mkoa wa Tanga unatekeleza miradi minne ya kusambaza umeme katika vijiji, miji, vituo vya afya, pampu za maji, maeneo ya migodi pamoja na viwanda vidogo ambayo thamani yake ni shilingi bilioni 137.87.

Amefafanua kuwa vijiji vyote 763 vya Mkoa wa Tanga mpaka sasa vimeshapata umeme kwa asilimia 100, pamoja na vitongoji 2,382 kati ya 4,531sawa na asilimia 52.6, navyo tayari vimewekewa umeme.

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Mhandisi Advera ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza katika Viwanja vya CCM Jitegemee wilayani Muheza mkoani Tanga, ambako Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea na ziara yake leo Februari 27,2025.

Ameongeza kuwa vitongoji 853 abavyo havina umeme vitapelekewa umeme katika kipindi cha miaka mitano na kwamba vitakavyobaki vitapelekewa umeme kulingana na utaratibu utakaokuwa umewekwa.
 
Back
Top Bottom