Pre GE2025 Tanga: REA waendelea kusambaza mitungi za gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma kampuni ya Manjis Logistics Limited ambaye atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Tanga kwa kuuza kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.

Hayo yamebainishwa Machi 01 , 2025 mkoani Tanga na Msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi wakati wa usimamizi na utekelezaji wa mradi wa usambazaji mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Mkomi amesema kuwa mitungi ya gesi 26,040 itakayosambazwa mkoani Tanga itachochea kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.

"Lengo la mradi ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kulinda afya za watanzania, kuboresha uchumi na kutunza mazingira ambayo yamekuwa yakiharibiwa kutokana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia.


Mkomi ameongezea kuwa, ili kurahisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Serikali imetoa ruzuku kwenye mitungi ya gesi ya kilo sita 3,255 kwa kila wilaya na mwanachi atatakiwa kuwa na kitambulisho chake cha Taifa ( NIDA) pamoja na pesa taslimu shilingi 17,500 tu.


Mkomi amesema, Serikali kupitia REA imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ikiwemo gesi (LPG) katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa mji na katika mkoa wa Tanga kiasi cha shilingi milioni 455.7 kimetengwa kutekeleza mradi.

Amezitaja wilaya zitakazonufaika kuwa ni pamoja na Wilaya ya Muheza, Korongwe, Bumbuli, Handeni, Lushoto, Pangani, Kilindi na Mkinga .

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya kicheba, Mhe. Khamisi Muhina ameipongeza REA kwa kuja na mradi huo na kuiomba iwe endelevu ili iweze kuwasambazia wananchi wengi nishati hiyo muhimu.

Source: BananaFm
 
Ikiisha gesi wanajaziwa bure au gesi haiishi? Aisee hili taifa lina maviongoz taka taka kbs aisee hapo ukute hata huko inakogawiwa hakuna hata duka lenye gesi kwmb ukabadilishe gesi ikiisha
 
Cha maana ni kushusha Bei ya kujaza gesi walau iwe sh. 10,000= mengine yoote ni maigizo tu , maana gesi itaisha na mitungi itakuwa vigoda vya kukalia tu, fuatilieni mlikogawa mitungi siku za nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…