Uchaguzi 2020 Tanga tuna jambo letu, Tanga imeamua, Tanga ni ya kijani

Uchaguzi 2020 Tanga tuna jambo letu, Tanga imeamua, Tanga ni ya kijani

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,830
Reaction score
972
Watanzania,

Salaam nyingi kwenu. Ninawapenda.

Mimi ni mtanzania ninayetokea mkoa wa Tanga. Leo ninataka kuongea na ninyi kuhusu Tanga. Wapo wasiojua, Ila wapo wanaoujua Ila wameamua kupotosha ukweli. Ni rahisi sana kusikia watu wa Tanga ni wavivu, washirikina, sio wasomi na mengine mengi mabaya. Ila kwa hakika sifa moja ambayo utaisikia ni kuwa "watu wa Tanga wanajua mapenzi". Sijajua ni kwanini mengi mazuri kuhusu Tanga hayatajwi.

Kipindi nchi hii inapata uhuru, Tanga ndio ulikuwa mkoa wa pili kwa maendeleo ukiacha Dar es Salaam. Anguko la uchumi wa Tanga lilitokana na anguko la zao la katani duniani baada ya kuibuka kwa manila.

Kwa taarifa yenu, kwasasa, Tanga ndio mzalishaji mkubwa wa mkonge Afrika. Nchi yetu inapata fedha za kigeni kutokana na mauzo ya mkonge nje ya nchi. Hapa Tanga tunao matajiri ambao utajiri wao umetokana na zao la mkonge/katani. Karibuni tuwekeze pamoja.

Tanga ndio mkoa unaoongoza Tanzania kwa uzalishaji wa matunda. Wilaya zetu mbili za Muheza na Lushoto zinatubeba sana. Kwa mfano ukiongelea machungwa Tanzania, unaongelea Muheza.

Kwa wale wasiofahamu, Tanga tunalima chai na tangawizi. Bumbuli na Amani ni maeneo yanayolimwa mazao hayo kwa wingi. Wilaya zetu za Handeni, Kilindi na Korogwe zinazalisha mahindi kwa wingi. Tunayo machimbo ya madini ya vito mbalimbali huko Korogwe na Mkinga.

Kama haitoshi, tuna hifadhi ya taifa ya Saadani huko Pangani. Saadani ni hifadhi inayoshika namba 13 kwa ukubwa na ni hifadhi ya kipekee kwani ndio hifadhi pekee inayopatikana pembezoni mwa bahari ya Hindi.

Tanga ndio nyumbani kwa mapango maarufu duniani, mapango ya amboni. Nakushauri fanya utalii wa ndani utembelee mapango haya ambayo licha ya uumbwaji wake wa kipekee, Ni mapango yenye historia ya kusisimua. Utasikia mengi kuhusu Salle (Osale) Otango.

Tanga tuna bandari kubwa ukiacha bandari ya Dar es Salaam. Bandari kubwa Tanzania, ni Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Saruji bora kabisa Tanzania, Tanga Cement, inatoka Tanga. Sasa tuna sungura. Kiwanda cha rhino. Chokaa Bora zaidi Tanzania, inatoka Tanga. Nadhani umeshawahi kusikia kuhusu Liemba.

Tanga tumezungukwa na bahari ya Hindi. Wilaya zetu tatu za Tanga, Pangani na Mkinga zimepakana na bahari ya Hindi. Tunavua samaki na hii ni moja kati ya shughuli zetu kuu za kiuchumi.

Hayo niliyoyataja hapo juu, yqnawezekanaje kutokea kwa watu walozi, wavivu na wasio na elimu?. Wapuuzeni wote wanaoisema vibaya Tanga.

Njooni mtembee, muione Tanga. Mkoa wa Tanga umebarikiwa kuwa na watu wakarimu sana. Ukarimu wetu ndio chanzo Cha msemo "waja Leo waondoka leo". Msemo huu sasa umehuishwa na kuwa "Karibu Tanga, kuondoka majaaliwa". Misemo hiyo maana yake ni moja tuu: ukifika Tanga hutataka kuondoka kutokana na uzuri na ukarimu wa watu wake.

Hali zote za hewa zinapatikana mkoani Tanga, kuanzia joto Kali, joto la kiasi, baridi ya kiasi mpaka baridi kali.

Sina hakika, lakini nadhani ukiacha Dar es Salaam, Tanga inaweza kuwa ndio mkoa unaofuata kwa kuwa na mtandao mkubwa wa barabara za lami. Tanga ndio mkoa unaoongoza kwa kuwa na huduma bora za maji. Mamlaka ya maji Tanga, Mara kwa Mara ndio inakuwa mamlaka bora ya maji Tanzania.

Tanga in mchango mkubwa Sana katika kupika na kuivisha masheikh wakubwa na maaskofu wakubwa wa Tanzania. Maaskofu wengi wa anglikana wanatoka Tanga. Kwa wasiojua, hata mchungaji Dkt. Fernandes ni mtoto wa Tanga.

Yule mama shujaa aliyekuwa nyuma ya Rais Magufuli katika mapambano ya ugonjwa wa korona, Ummy Mwalimu ni zao letu. MwanaFa - ni mtoto wetu, Juma Aweso - kijana wetu, makamba (senior and junior) - wanatanga. Orodha nii kubwa:
Mwakinyo
Matumla
Matonya
Kassim na wengine wengi.

Shule zilizopo Tanga Kama vile Galanos, Korogwe Girls na Tanga Tech, zimeelimisha wengi Kama Tundu Lissu na Zitto Kabwe.

Kwavile Tanga ni wakarimu, wajanja na walipa fadhila, mwaka huu ni kijani tuu ndio itatawala.

Amani Msumari
Tanga
 
Umeniudhi tu kumtaja mgombea moja anayetumiwa na Mabeberu hapo, umechafua uzi
 
Umeniudhi tu kumtaja mgombea moja anayetumiwa na Mabeberu hapo, umechafua uzi
Hao wawili nimewataja kwa makusudi.

Tunao akina Jakaya Kikwete, Dr. Asha rose Migiro, Mwiguli Nchemba n.k

Usiwaze sana jombii
 
Kuna mabeberu ya "kienyeji " yameitafuna hii nchi kuanzia inapata uhuru, haya ndio tunapaswa tuanze kuyatoa kwenye vitu.
Umeniudhi tu kumtaja mgombea moja anayetumiwa na Mabeberu hapo, umechafua uzi
 
Wilaya ya muheza imepakana na bahari pia mkuu..najua kuna watu hawajui hili.
 
Tanga haitakaa iinuke tena mpk siku wenyeji mkiacha kutumia ngono zembe kama kivutio Cha watu kuja Tanga.
 
mkuu mbona hujamtaja juma ramadhani mgunda..hujaitaja coastal union wana mangush!!
 
Umesema Tanga ndiyo mzalishaji mkubwa wa mkonge katika Afrika?
Ningependa kujua Tanzania inashika nafasi ya ngapi ktk Afrika.
 
Back
Top Bottom