Tanga: Utaratibu wa ugawaji mahindi ya msaada unatukera, Serikali iangalie utaratibu uliopo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wanakijiji Tanga wanapanga foleni kupata msaada wa mahindi na pia lazima waje na vitambulisho, wanauziwa kilo moja kwa shilingi mia tisa, watu ni wengi sana na foleni huenda ikawa hadi jioni na kitu endelevu.

Kinachofanyika kwa sasa kimekuwa kikifanyika wiki nzima yote hii. Wanaunganika wanavijiji wa Handeni kupata huduma huu, kinachosikitisha zaidi ni kuwa mtu anaweza kumaliza saa kadhaa kukaa kwenye foleni.

Wao wanasema ni mahindi ya msaada lakini kwamba kuna mtu kajitolea kuwapa lakini masharti ya kuyapata ni mengi na lazima uwe na utambulisho wa Kijiji ndio unahudumiwa.

============

Mkuu wa Wilaya aelezea
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe anasema: “Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na wenzetu wa World Vision wakishirikiana na Wizara waliona kuna kata zina upungufu wa chakula, changamoto ambayo imetokana na ukame wa mvua katika maeneo mengi.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na changamoto hiyo aliamua kutupatia msaada wa chakula tani 100 za mahindi ya bei nafuu, tukagawa yakaisha.

“Jana (Novemba 23, 2022) tulipokea mahindi mengine tani 100, hayo yanauzwa ambapo mwananchi anakuwa ameokoa Tsh. 420 kwa kila kilo moja, zoezi la ugawaji linaendelea hadi sasa.

“Kuhusu madai ya kuwepo kwa foleni kubwa na utaratibu mwingine wa ugawaji chakula naomba wanaojua hilo ni NFRA (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula), wao ndio wanaoweza kutoa taarifa rasmi.”

Ufafanuzi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
Valeria Mwenda wa NFRA anasema: “Kwa siku nawapimia watu hadi 150, anayepokea chini zaidi ni anayepokea kilo mbili, natumia mkono kupima, foleni ipo lakini sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kukaa kwa saa kadhaa.

“Changamoto iliyopo hapa, watu hatupeani ushirikiano, kila mtu akija anataka kuwa wa kwanza, mwisho wa idadi ya kilo kw amtu mmoja ni kilo 100, wengine wanataka zaidi ya kilo 100 ukiwakatalia wanalalamika.

“Hapa hatutuo mahindi kwa ajili ya kwenda kuuzwa bali kwenda kutumiwa na wananchi, hivyo kuna wengine wanaokuja kwa lengo la kuchukua mahindi ya biashara, wakikwama ndio wanalalamika.

“Hapa kwa siku napima hadi tani 19 kwa siku, natumia mkono, naweza kujiuliza hiyo kazi ni kubwa kiasi gani.”
 
Wanagawa mahindi ya msaada?

Si ni jana tu mamaenu kasema chakula kipo cha uhakika? Hata siku mbili hazijapita, tayari foleni za mahindi ya msaada zimeanza?
 
Nchi imetafunwa kwa muda mfupi balaa. Tunawazidi hadi kenya kwa njaa
 
Mwananchi mmoja mmoja tuweke au tuanzishe utaratibu wa kuwa na akiba angalau ya miezi 3-6

Piga hesabu ujue matumizi ya nyumbani kwako, ongea na familia yako, nunua vyakula weka.

Ila kuwa makini kuna wajinga wataweza gawa akiba ya familia, hivyo Baba anatakiwa aiweke Akiba mbali kabisa na funguo awe nazo yeye pekee

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wanakijiji Tanga wanapanga foleni kupata msaada wa mahindi na pia lazima waje na vitambulisho, wanauziwa kilo moja kwa shilingi mia tisa, watu ni wengi sana na foleni huenda ikawa hadi jioni na kitu endelevu.

Kinachofanyika kwa sasa kimekuwa kikifanyika wiki nzima yote hii. Wanaunganika wanavijiji wa Handeni kupata huduma huu, kinachosikitisha zaidi ni kuwa mtu anaweza kumaliza saa kadhaa kukaa kwenye foleni.

Wao wanasema ni mahindi ya msaada lakini kwamba kuna mtu kajitolea kuwapa lakini masharti ya kuyapata ni mengi na lazima uwe na utambulisho wa Kijiji ndio unahudumiwa.

============

Mkuu wa Wilaya aelezea
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe anasema: “Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na wenzetu wa World Vision wakishirikiana na Wizara waliona kuna kata zina upungufu wa chakula, changamoto ambayo imetokana na ukame wa mvua katika maeneo mengi.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na changamoto hiyo aliamua kutupatia msaada wa chakula tani 100 za mahindi ya bei nafuu, tukagawa yakaisha.

“Jana (Novemba 23, 2022) tulipokea mahindi mengine tani 100, hayo yanauzwa ambapo mwananchi anakuwa ameokoa Tsh. 420 kwa kila kilo moja, zoezi la ugawaji linaendelea hadi sasa.

“Kuhusu madai ya kuwepo kwa foleni kubwa na utaratibu mwingine wa ugawaji chakula naomba wanaojua hilo ni NFRA (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula), wao ndio wanaoweza kutoa taarifa rasmi.”

Ufafanuzi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
Valeria Mwenda wa NFRA anasema: “Kwa siku nawapimia watu hadi 150, anayepokea chini zaidi ni anayepokea kilo mbili, natumia mkono kupima, foleni ipo lakini sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kukaa kwa saa kadhaa.

“Changamoto iliyopo hapa, watu hatupeani ushirikiano, kila mtu akija anataka kuwa wa kwanza, mwisho wa idadi ya kilo kw amtu mmoja ni kilo 100, wengine wanataka zaidi ya kilo 100 ukiwakatalia wanalalamika.

“Hapa hatutuo mahindi kwa ajili ya kwenda kuuzwa bali kwenda kutumiwa na wananchi, hivyo kuna wengine wanaokuja kwa lengo la kuchukua mahindi ya biashara, wakikwama ndio wanalalamika.

“Hapa kwa siku napima hadi tani 19 kwa siku, natumia mkono, naweza kujiuliza hiyo kazi ni kubwa kiasi gani.”
fanyeni kazi mamwinyi nyie muache kuomba omba misaada na kutoa masharti ya namna gani mpewe chakula. acheni kushinda kutwa mnapiga soga na kucheza bao.
 
Back
Top Bottom