Tanga: Watendaji Bodi ya Mkonge wahukumiwa kwa Matumizi mabaya ya Mamlaka

Tanga: Watendaji Bodi ya Mkonge wahukumiwa kwa Matumizi mabaya ya Mamlaka

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Septemba 13, 2022 iliwahukumu Shabani Mapinda aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi na Imani Mduruma aliyekuwa Meneja wa Bodi ya Mkonge Nchini kifungo cha mwaka Mmoja jela kwa matumizi mabaya ya Mamlaka.

Katika Shauri la Uhujumu Uchumi Namba ECC 06/2022, washtakiwa walipatikana na hatia ya kufanya uhamishaji wa shamba lililokuwa la Bodi ya Mkonge ( Farm no. 733/2) lililopo eneo la Hale wilayani Korogwe, kwenda kwa Kampuni ya HBU Katani Limited bila ya kuishirikisha Bodi ya Wakurugenzi.

Kila mshtakiwa ametakiwa kutumikia kifungo cha Mwaka Mmoja jela huku shamba hilo likiamriwa kurudishwa kwa Serikali.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Septemba 13, 2022 iliwahukumu Shabani Mapinda aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi na Imani Mduruma...
Angalau kidogo serikali ya Rais Samia inaonekana kudeal na mafisadi. Ile nyingine ilijikita kupambana na Chadema tu.
 
Back
Top Bottom