Tanga: Watu 5 wamekufa kwenye ajali ya Vuga Lushoto

Tanga: Watu 5 wamekufa kwenye ajali ya Vuga Lushoto

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Watu watano wamefariki na wengine wanane wamejeruhiwa baada ya basi dogo aina ya Toyota Coaster kuacha barabara na kutumbukia bondeni katika eneo la Vuga, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga.

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 18, 2026, majira ya saa 7:30 mchana katika barabara ya Mombo-Lushoto. Gari hilo, lenye namba za usajili T.151 DMC, lilikuwa likitokea Tanga Mjini kuelekea Ngwashi na lilikuwa likiendeshwa na Ally Dione.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema watu waliopoteza maisha ni wanaume wawili wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 hadi 45, wanawake wawili wenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 25 na 35, pamoja na mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita. Majina yao hayajafahamika bado. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa ajili ya uchunguzi, utambuzi na taratibu nyingine za kisheria.

Waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Soni, Lushoto.

Uchunguzi wa awali wa Polisi umebaini kuwa ajali hiyo huenda imesababishwa na uzembe wa dereva na kushindwa kulimudu gari.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini mazingira kamili ya ajali hiyo na wametoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.
IMG-20260818-WA0039.jpg
 
Daah ile njia aiseee, alafu dereva anakimbiza gari unajiuliza tukienda kule bondeni si ntakuwa chapati mimi.
Poleni wafiwa!!!!!
 
Poleni sana mliopoteza wapendwa wenu
 
Back
Top Bottom