Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza kukamatwa kwa wasimamizi wa Mradi wa Maji Kwamsisi, katika kata ya Kwamsisi ili uchunguzi ufanyike kutokana na kuhisiwa vitendo vya ubadhirifu wa fedha zilizokusanywa kutokana na malipo ya wananchi.
Waziri Aweso ametoa agizo hilo siku ya Jumatatu Desemba 23, 2024 katika kata ya Kwamsisi, wilayani Handeni mkoani Tanga kutokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kumtaka Aweso ahakikishe changamoto ya upatikanaji wa maji safi katika eneo hilo inatatuliwa.
"Katibu anayeendesha mradi anasema kuna Shilingi milioni mbili, Mhasibu anasema kuna milioni nane, Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi ninamuuliza mradi wake una vituo vingapi vya maji anasema hajui, ninamuuliza kwenye akaunti kuna kiasi gani anasema kuna milioni 3, benki tumewauliza wanasema kuna elfu 30 tu", ameeleza Aweso.
Halikadhalika ameagiza kuvunjwa kwa kamati ya mradi huo kutokana na madai hayo ya ubadhirifu, na kumuagiza Mkuu wa Wilaya kufuatilia iwapo fedha zilizopelekwa kuboresha huduma ya maji katika eneo hilo zimetumika kama zilivyokusudiwa.