Ongea kwa data, mimi nimeongea kwa data juu Tanga ni mkoa wa Tatu Tanzania nzima kwa viwanda, nchi nzima mnasubiria Tanga kwanza Tusage Mawe, tukimaliza tutengeneze poda halafu Tu supply viwandani mtengeneze Rangi, Grout za Tiles na vinginevyo, karibia kila nyumba unayoiona Nchi hii part imetumika nguvu ya watu wa Tanga. Hapa naongelea Neelkhant na Maweni source ya karibia poda yote Nchi nzima.
Sisi tukasababisha msipauke, wengi hamuwezi kununua vipodozi vya nje, Vipodozi vya ndani karibia vyote kuanzia Baby care, Vasteline, Cocoa Butter, Family care, skala, podoa etc in short hakuna wilaya utaingia dukani usikute vipodozi vya Tppl ama Mamujee.
Unapoongelea Investment kubwa na matajiri wakubwa kama kina Gsm, Shoppers, Hao kina Home shopping, Bin slum, Oil Com etc wote asili yao ni Huko Tanga. Na hata ambao hawatoki Tanga kama Kina MO na Bakhresa utakuta wana strong connection huko.
Hapo Bado cement, Matunda, umeme, spices na vitu kibao.
In short kuuita mkoa ambao kila mwaka upo Top 10 ya kuchangia pato la Taifa kama wa wavivu ni "uvivu" wa kufikiri.