Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Ikiwa siku chache zimepita tangu tulivyoripoti taarifa kuhusu wananchi wa Bondo, Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga kulia kukosa makazi baada ya nyumba zao kuchomwa moto na kubomolewa kwa kuambiwa wamevamia hifadhi.
Inakadiriwa kuwa zaidi ya kaya 2,600 zimeachwa bila makazi, mali zao kuharibiwa, na familia zao kutawanyika, huku wengine wakiwa hawajui walipo wapendwa wao, ikiwemo watoto wadogo.
Tukio hili linahusishwa na operesheni ya kuwaondoa wananchi hao kwa madai ya kuvamia eneo la hifadhi ya msitu. Kwa mujibu wa mashuhuda, usiku wa tarehe 3 Januari ulikuwa wa mateso yasiyosahaulika, baada ya vikosi vya ulinzi vilivyojihami kwa silaha kuingia eneo hilo na kuanza kuwafurusha kwa nguvu. Inadaiwa kuwa mabomu ya machozi, risasi na moto vilitumika katika kuwaondoa wakazi hao, huku wengine wakidai kupigwa, kuteswa na hata wanawake kubakwa mbele ya watoto wao.