Tanganyika black people hawakuwa Citizens

Tanganyika black people hawakuwa Citizens

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Hivi nini Watanzania hujiita Watanganyikwa wakati ukweli ni kwamba hawakuwa raia wa Tanganyika? Wahindi na Waarabu ndio waliokuwa citizens wa nchi ya Tanganyika.

Mtu mweusi amepata citizenship mara ya kwanza baada ya 1961.

Sasa kwa nini mnajiita Watanganyika wakati hamjawahi kuwa citizens wa Tanganyika?

Watu kama Issa Shivji ndio waliokuwa Watanganyika au citizens wa Tanganyika lkn siyo wewe, …
 
Hao Wahindi na waarabu waliokuwa watanzanja si tuko nao humu!!!

Walioondoka humu hawawezi kuwa Watanzania.
 
hao wahindi na waarabu waliokuwa watanzanja si tuko nao humu!!!

walioondoka humu hawawezi kuwa watanzania.

Lakini Wahindi wote ni Watanganyika watu weusi hawajawahi kuwa Watanganyika!
 
Screenshot_20221025-174613.png

Aya ya kwanza unadai watu weusi hawakuwa Watanganyika.

Aya ya pili ukajibu kwamba watu weusi walipata uraia wa Tanganyika mwaka 1961.

Sasa Kijakazi kuna swali tena?
 
..tulikwenda Umoja wa Mataifa kudai Uhuru wa nchi inayoitwa Tanganyika.

..Dec 9, 1961 tulipandisha bendera na kutangazwa kuwa taifa huru.

..Vilevile tuliandikishwa uanachama ktk umoja wa mataifa na jumuiya mbalimbali kama Tanganyika.

..Tanzania ni zao la Tanganyika na Zanzibar.
 
Nyerere wakati anaenda UNO...niishie hapo kwanza.
 
Hivi nini Watanzania hujiita Watanganyikwa wakati ukweli ni kwamba hawakuwa raia wa Tanganyika? Wahindi na Waarabu ndio waliokuwa citizens wa nchi ya Tanganyika.

Mtu mweusi amepata citizenship mara ya kwanza baada ya 1961.

Sasa kwa nini mnajiita Watanganyika wakati hamjawahi kuwa citizens wa Tanganyika?

Watu kama Issa Shivji ndio waliokuwa Watanganyika au citizens wa Tanganyika lkn siyo wewe, …

MAPAMBANO YANAENDELEA ALUTA CONTINUA DHIDI YA ALIOHODHI MADARAKA BAADA YA 'UHURU'

Hatuwezi kujisifia wale kujipiga vifuani kwa kuwa sasa kuna 'mkoloni mweusi' aliyetengeneza matabaka na kujipendelea wao wachache ndani ya vyama vya 'ukombozi' bila kujali madhila wanayopitia wengi kwa miaka 61 ya uhuru wa bendera .

Wakoloni wote wawe wa sasa yaani wanaojiita vyama vya ukombozi vilivyoleta uhuru au wakoloni wakongwe au wawe WaOmani, Waingereza, Portuguese, WaJeremani n.k wote ni watesi kwa namna zote...

Kuwa sasa tunatawaliwa na chama kilicholeta uhuru lakini kina ubaguzi wa kisiasa, ubaguzi kwa kuweka tabaka la elimu, ubaguzi katika bima ya afya mfano wabunge wana bima maalum ya kwao, ubaguzi wa huduma za maji safi na salama, ubaguzi kwa kujipendelea maghari ya kifahari V8 wakati huduma za afya, elimu zinakosa fedha kwa ajili walio wengi raia wa kawaida.

Kwa muktadha huu nchi hii Tanzania, Tanganyika, Zanzibar kuna matabaka yanaendelea na hakuna la kujisifia baada ya uhuru wa bendera na mapinduzi.

Samora Machel : Ukoloni wa kiFikra

Katika hotuba yake motomoto kuhusu kutawaliwa, alihoji vipi mwafrika aliyetawaliwa na mfaransa akajiona m-bora kuliko mwingine kwa kuwa Ufaransa wana tamaduni bora zaidi ya uandishi wa mistari ya mashairi ya mapendo kwa umahiri wa kisomi.

Samora Machel anazidi kuwaza hata wale waliotawaliwa na muingereza wajiona wao ni bora kwa vile Uingereza ilitawala nchi nyingi zaidi na inasemekana ni wazungu 'wastaarabu' zaidi.

Samora Machel anatuasa ingawa Portugal ni nchi masikini zaidi ktk ulaya lakini ni nchi iliyoendekeza ukoloni kama Ufaransa, Uingereza na Ureno / Portugal na sifa za nchi zote hizo za ulaya ni kuwa ziliendekeza ukoloni.

Samora Machel anapigia mstari neno ukoloni na kuwa ukoloni ni unyama hauna utu hivyo kujisifia wewe ni zao la ukoloni huu au ule wenye hadhi ya juu ni kukosa fikra sahihi.

Hivyo maneno ya Samora Machel anasisitiza tuamke na kuwa mapambano lazima yaendelee (2022) dhidi ya ukabila, ujinga, maradhi, njaa, ushirikina na mawazo potofu ya kukumbatia ukoloni wa aina yoyote.

Samora Machel anakumbushia kuwa Mozambique walipambana na ukoloni mkongwe wa miaka 500 uliokuwapo Mozambique, na kama kawaida pamoja na umasikini wa taifa la Portugal barani ulaya,lakini walikuwa wakoloni kama wakoloni wengine. Nchi za France, Uingereza, Holland, Germany, Portugal, Italy zote zilikuwa na makoloni. Mataifa mengine kama Oman n.k pia yalikuwa na makoloni yake kule Persia, Pakistan, Emirates, Congo, Burundi, Somalia, Kenya, Tanganyika, Zanzibar, Mozambique .

Anamalizia kuwa ukoloni wowote hauna usafi wa kujivunia kwani ni Ukoloni unaogandamiza jamii zingine na kuzigawanisha.
 
Hivi nini Watanzania hujiita Watanganyikwa wakati ukweli ni kwamba hawakuwa raia wa Tanganyika? Wahindi na Waarabu ndio waliokuwa citizens wa nchi ya Tanganyika.

Mtu mweusi amepata citizenship mara ya kwanza baada ya 1961.

Sasa kwa nini mnajiita Watanganyika wakati hamjawahi kuwa citizens wa Tanganyika?

Watu kama Issa Shivji ndio waliokuwa Watanganyika au citizens wa Tanganyika lkn siyo wewe, …
Duh ! Na baada ya Uhuru hao wahindi na waarabu wakaitwa British subject kwanini ?!
 
Ni vyema Marijuana ikakaushwa kabla ya kuvutwa,mbichi ina madhara kwa afya ya akili.
 
Back
Top Bottom