iArmaniAdamson
iArmaniAdamson,
Unaniambia nisome vitabu vya historia nijifunze maisha yalivyokuwa Zanzibar.
Kuna uongo mwingi sana katika vitabu vya historia ya Zanzibar na takriban
nimesoma vyote.
Licha ya kusoma nimeshiriki pia kama mtafiti msaidizi wa Dr. Harith Ghassany
wakati anaandika kitabu chake: Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.
Kitabu hiki ndicho ''corrective,'' katika vitabu vyote kuhusu historia ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Anza kupita hapa ili tufahamiane vyema:
Mohamed Said: KUTOKA ZANZIBAR DAIMA: VIDOKEZO NA VIONJO KATIKA UANDISHI WA KWAHERI UHURU KWAHERI UKOLONI
(Zanzibar Daima wamekosea ni: Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru).
Mimi si kuwa tu nimesoma mengi katika historia ya Zanzibar bali nimezungumza
kwingi na kuandika mengi kuhusu Zanzibar.
Baba yangu alikuwa karibu sana na vijana wenzake wa Zanzibar wakati wa
siasa za kudai uhuru na baadhi yao waliuawa baada ya mapinduzi.
Hivyo basi sizungumzi haya kama mtu wa nje.
Nina mengi nimeyajua bila hata ya kusoma vitabu.
Ingia hapo chini tufahamiane:
Mohamed Said: Obituary The Weeping and Whipping Pen of Ali Mohamed Nabwa 1936 -2007
Mohamed Said: KUULIWA KWA ABDALLAH KASSIM HANGA
Mohamed Said: SIKIZA KIPINDI MAALUM: MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA 1964
Kuhusu mpango wa Jamshid kuja kutawala Zanzibar sidhani kama hili linastahili
sisi kulijadili.
Jamshid ni kikongwe hivi sasa.
Umerudia tena lugha za kibaguzi ambazo hivi sasa hazina nafasi katika Zanzibar
ila kwa kikundi cha mahafidhina wachache ndani ya CCM Zanzibar.
Lugha yako ni lugha ya Kisonge ambayo badala ya kujenga madaraja inajenga
kuta na kueneza siasa za chuki katika jamii ya Wazanzibari.
Prof. Ibrahim Noor kaeleza tatizo hili katika kitabu chake: Tanzania na Propaganda
za Udini.
Angalia hapo chini:
Mohamed Said: KITABU KIPYA: TANZANIA NA PROPAGANDA ZA UDINI NA PROF. IBRAHIM NOOR
Kwa kumalizia napenda nikueleze kuwa wazee wetu waliasisi Zanzibar Nationalist
Party (ZNP) ili kujenga utaifa.
Lengo lilikuwa kujenga taifa moja la Wazanzibari.
Ndugu yangu hii leo wewe unajitahidi kuturudisha nyuma kwa lugha za kibaguzi
za ''ugozi'' kwa kutafuta makabila ya watu na rangi zao.
Hii ni fitna.
Insha Allah chukua muda nisome na nisikilize katika audio nilokuwekea hapo juu.
Hili sasa ni darsa endelevu In Sha Allah ili sote tufaidike.
Nina mengi.
PS: Hilo la elimu yako sikulijibu kwa kuwa halikutoka kwangu.