Tanganyika groundnuts scheme na sakata la mafuta ya kula

Tanganyika groundnuts scheme na sakata la mafuta ya kula

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Wakati wa vita ya pili ya dunia Uingereza ilipatwa na upungufu mkubwa sana wa mafuta ya kula. Wakakaa chini wakaumiza vichwa wafanye nini. Wakakubaliana kulima karanga kwenye koloni lao la Tanganyika. Mipango ikafanywa, eneo linalofaa likatafutwa, wakapata huko Kondoa. Wakanunua matrekta wakajenga kambi na maandalizi yote ya kilimo.

Mpango wao huo ulifeli vibaya sana. Kwanza kusafirisha matrekta na magreda ilikuwa kazi sana. Walikuta mto Ruvu umefurika. Huko eneo la kazi mvua ya mafuriko ilipiga sana. Pia mashine walizoleta zilikuwa hazina uwezo wa kung'oa mibuyu na wale wataalamu wa kitanganyika hawakuwa na ujuzi wa kuziendesha. Ishi hii ilizua kelele nyingi sana katika bunge la Uingereza. Walipata somo la kutokurupuka.

Somo ninalopata mimi kwenye kisa hiki ni uthubutu na watu kuumiza kichwa ili kutatua matatizo. Kufanya mambo kwa mazoea hakujawahi leta utatuzi wowote wa matatizo. Kuthubutu ni afadhali kuliko kukaa idle ukidhani mambo yatajisolve.
 
Back
Top Bottom