Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kuna wakati huwa nashangazwa Sana na mawazo ya baadhi ya wazanzibari wanapoona kuwa Tanganyika inafaidika zaidi na Muungano kati yake na Zanzibar, kuliko Zanzibar inavyofaidika na Muungano huo.
Wazanzibari hao ndiyo waliobuni msemo wa "Tanganyika imevaa koti la Muungano" kumaanisha kuwa Muungano unaendeshwa na Tanganyika Kwa faida yake na zanzibar hawana wapatalo.
Lakini hiyo Tanganyika ambayo inasemwa imevaa koti la Muungano Iko wapi? Nani anaweza kuonesha mipaka ya Tanganyika na nchi nyingine?
Mipaka ya Zanzibar iko na inajulikana na wenyewe wazanzibari wanataka iheshimiwe. Mipaka inayoitambulisha nchi ya Tanganyika iko wapi?
Zanzibar Wana Serikali Yao Kamili na timilifu inayosimamia mambo ya Zanzibar. Serikali ya Tanganyika iko wapi?
Zanzibar wanao utambulisho wao na hata uraia wa Zanzibar ni kwa ajili ya wazanzibari. Uraia wa Tanganyika unapatikana wapi na kivipi?
Muungano umeiua Tanganyika na kuizika Tanganyika kwenye kaburi la Muungano na kuiacha hai Zanzibar pekee.
Soma Pia: Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar?
Tanganyika iliyouliwa na Muungano inawezaje kuvaa koti la Muungano? Uliona wapi marehemu akawa na uwezo wa kujivalisha nguo?
Kama kuvaa koti la Muungano basi Zanzibar ndiyo yenye uwezo wa kuvaa koti la Muungano na si Tanganyika. Maana Zanzibar iko hai.
Hebu angalia Mzanzibari anavyopata Kila haki anayopata Mtanganyika lakini Mtanganyika hawezi kupata Kila haki anayopata Mzanzibari, kutokana na yeye kuwa Mzanzibari ndani ya Muungano.
Na bahati mbaya sana CCM haina ubavu hata nukta wa kupigania kufufuliwa Kwa Tanganyika Wala kupigania mirathi ya marehemu Tanganyika.
Wana CCM wanaotokana na Marehemu Tanganyika, hawana ubavu wa kufurukuta dhidi ya wanzibari wana CCM linapokuja suala la kuivua Zanzibar koti la Muungano.
Wajinga ndiyo waliwao.