Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kabla ya Tanzania kulikuwa na Tanganyika, na kabla ya Tanganyika ilibaki kidogo kuwe na Windsorland, yaani nchi ya Windsor.
Ni hivi
Kabla ya yote hayo hakukuwa na nchi moja kama ilibyo sasa. Kulikuwa na tawala ndogo ndogo nyingi ambazo kila moja iliishi kama nchi inayojitegemea, chini ya machifu wao.
Baada ya mkutano wa Berlin wa 1884, mataifa ya Ulaya yakamwagika Afrika kugawana ardhi ya kutawala.
Mjerumani akaja eneo hili na kuwapora ardhi wale machifu na kuziunganisha ili kuunda nchi moja.
Nchi hiyo ikaitwa Ujerumani ya Afrika Mashariki, na mipaka yake ni eneo lote la Tanzania bara ya sasa, Rwanda, Burundi pamoja na eneo la Quionga ambalo sasa ni sehemu ya Msumbiji.
Ikatokea vita vya kwanza vya dunia, 1914-18 ambayo Mjerumani alishindwa. Akanyang'anywa maeneo yote aliyokuwa akiyatawala, ikiwemo ile nchi ya Ujerumani ya Afrika Mashariki.
Nchi hiyo ikachukuliwa na Mwingereza, na jambo la kwanza likawa kubadili jina lile la kirejumani.
Ukaanza mchakato wa kutafuta jina jipya na majina kadhaa yakapendekezwa.
Kulikuwa na jina la Smutsland, kwa heshima ya Jan Smuts, kamanda wa jeshi la Uingereza kutoka Afrika Kusini, aliyeongoza mapambano dhidi ya majeshi ya Ujerumani ndani ya Afrika Mashariki kwenye vita ya kwanza ya dunia.
Kulikuwa na majina mengine kama Eburnea, New Maryland na Victoria - kwa heshima ya Malkia Victoria.
Halafu kulikuwa na jina la Windsorland, ambalo limetajwa mwanzo kule.
Hili ni jina la nyumba na familia ya kifalme ya Uingereza.
Kwa kawaida, ufalme wowote unatoka kwenye nyumba fulani...au familia fulani, au ukoo fulani.
Ufalme wa Uingereza unatoka kwenye nyumba ya Windsor, ambako pia Malkia Elizabeth wa pili aliyefariki hivi karibuni, na mwanaye Charles wa tatu aliyerithi kiti, wanatoka.
Majina haya yakatumwa makao makuu London kwenye ofisi ya makoloni.
Waziri wa makoloni akayakataa yote akisema anataka maajina yenye asili ya nchi husika, badala ya majina ya kigeni.
Ndipo majina ya Kilimanjaro, Tabora na Tanganyika yakapendekezwa.
Kilimanjaro ilikuwa kwa heshima ya mlima, Tabora kwa heshima ya mji mkubwa wa kibiashara maeneo ya katikati
Jina la Tanganyika likapita na kuwa rasmi, Februari Mosi, 1920.