Tanganyika jeki..

Tanganyika jeki..

sexologist

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
2,276
Reaction score
976
Wadau naomba maana na asili ya hili neno. Toka nakua ninasikia flani kabebwa na polisi kutumia Tanganyika jeki.

Hivi hii Tanganyika Jeki ni nini na ina uhusiano gani na watu wanavyokamatwa, na ilianza lini? Hope ni kabla ya uhuru (najaribu kuhisia).

Wenye mawazo mapana zaidi yangu karibuni.

Muwasilisho wa asubuhi!
 
Ni aina ya jeki zilizokuwa zinatumika zamani kabla ya hizi za kisasa. Mpaka sasa unaweza kuziona na zinatumika sana kwenye magari ya kusafirisha watalii au yanayokwenda maporini kusiko na barabara au barabara zenye matope mengi. Najua kuna mtu atatupia picha humu jamvini.

Na sababu ya pili mtuhumiwa akishikwa maana yake anainuliwa kwa kushikwa suruali nyuma kiunoni na hapo atatembelea vidole na hatakuwa na uwezo wa kukimbia na ni rahisi kupigwa ngwara. Ndio maana watoto wa mjini wanaita Tanganyika jeki.
 
Back
Top Bottom