Tanganyika Law Society (TLS): Jeshi La Polisi limekosea katika kuzuia maandamano

Tanganyika Law Society (TLS): Jeshi La Polisi limekosea katika kuzuia maandamano

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869

🅻🅸🆅🅴 MWABUKUSI RAIS WA TLS ANAZUNGUMZA MUDA HUU.

Rais wa TLS mwanasheria Boniface Mwabukusi akiongoea na waandishi wa habari kuhusu hatua walizochikua kuzuia maandamano ya jana tarehe 23 September 2024 walikosea



Rais wa TLS akiongea na jopo la waandishi wabobezi nchini Tanzania mkurugenzi wa Jambo TV John Marwa, na muendesha kipindi aliyejizolea sifa kubwa nchini Chief Odemba wa Star TV waangazia masuala.

Kuhusu ushiriki wa TLS kutetea masuala mbalimbali ikiwemo maandamano, rais wa TLS anasema tunawaelewa sana na kuwakubali walioandaa maandamano na ndiyo maana ...

TLS tunavipongeza vyombo vya habari vya Jambo TV na Star TV kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa habari na pia kufanya mahojiano mazito ..... ni mfano wa kuigwa maana masuala ya nchi hii siyo jukumu la TLS ni la sisi wote kutoka sehemu mbalimbali za kijamii kujitoa kutimiza.

BONIFACE MWABUKUSI

Kuhusu kuchunguza mauaji na utekaji mauaji na utekaji, Rais raisi ana fursa ya kuunda tume huru na yenye credibility ili polisi wakae kando. Nchi inaw ate wengi wabobevu ambao wanaweza kusaidia katika hilo. Tulishaona Kikwete aliunde kitu cha namna hiyo na ilileta majibu na watu wakachukuliwa hatua.

Kwakuwa inatakiwa tupate majawabu, sidhani kama ni vizuri sana mtu anayelalamikiwa kujichunguza. Waganda wana msemo: A monkey can’t judge affairs of the forest.

Swali: Kumekuwa nan a mapendekezo ya CHADEMA na wengine kuhusu kuundwa kwa tume lakini Rais ameamua Polisi ambao wamekataliwa ndiyo wafanye uchunguzi. Unatehgemea matokeo gani?

Siwezi kujua tutapata matokeo gani kwakuwa sijaona Terms of Reference, ambayo inonesha wanaenda kuchunguza nini na ndiyo unaweza kujua utarajie nini. Na Rais sisi ni washauri wake tu, ana haki ya kupokea au kukataa. Ushauri si lazima ukubalike. Tunaposhauri ni kwa nia njema.

------
“Maandamano ni haki ya kisheria kama mtu anataka kupiga kapige wale wabunge waliotunga sheria sio mlaji wa ile sheria kama unafikiri maandamano ni uhalifu yaharamishe kisheria jenga hoja yaharamishe kisheria tutofautishe ghasia na maandamano unajau kuna vitu viwili watu hawatofautishi ghasia na maandamano.

Maandamano ni njia bora tu ya kueleza lakini watu ambayo wanazungumza kuonyesha hisia kwa pamoja kwa kutumia miguu mikono na wale wasiokuwa na miguu wanatembea lakini nia yao ni wafike mahala kueleza hisia kwa pamoja kwa hiyo maandamano siyo uhalifu ndio maana kwenye sheria ya vyama vya siasa ni moja ya haki ya chama cha siasa kufanya maandamano na polisi hawaruhusiwi kujiingiza kwenye usimamizi wa shughuli za kisiasa.

Anayeweza kuwambia polisi hiki kiko juu na zaidi ni msajili, sijamsikia mimi msajili akizungumza kwa sababu msajili anajua hivi vyama ni vyake na anajua sheria hizi ni zake na anaweza akasema kwamba kwa mwenendo huu hii siyo dhumuni la kile kifungu.

Lakini vilevile inabidi uangalie sababu hawa CHADEMA wanalalamikia watu kupotea wanataka kuandamana kwa ajili watu wanapotea hii sio sababu kisheria?.Je ile kutafuta watu waliopotea au kuandamana kushinikiza watu waliopotea hatua zichukuliwe wapatikane au tujue wako wapi kazi haramu? siyo kazi haramu ni kazi halali ya kulinda uhai wa mtu ambayo ndiyo jukumu la msingi la kwetu.

Nguvu kubwa ilitakiwa itumike kuwatafuta kina Azory Gwanda akina Ben Saanane, akina Simon Kaguye akina Soka na wenzake na wengine wote sisi tulitoa majina ya zaidi ya watu 84 na imeongezeka saivi kule ndiyo tupeleke nguvu huwezi kupeleka nguvu kumdhibiti anayelia bila kutafuta chanzo kinachomsababisha aliye”

------

Watanzania waambie njooni muandamane Simba ameleta kombe, wataandamana hata uchi kwenda uwanja wa Taifa. Wanazingatia sana mamboa ambayo si ya msingi.

Kwenye culture yetu tuliamini kuwa mambo yote magumu magumu ni ya viongozi. Hali hii itaendele na itakuwepo kwa muda mrefu kwasababu kwanza hatujabadili mfumo wetu wa elimu na sasa hivi tumeubemenda, tumeutikisa zaidi.

Ile free thinking huipati sawasawa ndiyo maana utakuta watoto wa siku hizi Ukimona anapiga kelele ni boom, yaani kama ndege.

Pia, soma:
 
Ujumbe uwafikie watawala wa serikali ya chama dola kongwe

1727179431632.png
 
Rais mstaafu wa TLS wakili msomi Bahame Tom Nyanduga apigilia msumari



View: https://m.youtube.com/watch?v=-rEB1KWiKXM

Advocate Bahame Tom Nyanduga, is a Tanzanian national who practices law in Tanzania, based in Dar es Salaam and a former Tanganyika Law Society president
 
Back
Top Bottom