Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimelaani tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa mwanachama wake Wakili Joseph Masanja lililotokea Babati Mkoani Manyara.
Kupitia taarifa iliyotolewa na chama hicho Disemba 28, 2024 imeeleza kuwa mwili wa marehemu Wakili Masanja uliokotwa eneo la Bwalo la Magereza, Manyara na alifariki siku ya jumatatu tarehe 23/12/2024 jioni katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya KCMC alipopelekwa kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Soma pia: TANZIA Wakili kesi ya Gekul afariki dunia Desemba 24, 2024
TLS imevitaka vyombo vinavyohusika na uchunguzi vichukue hatua za haraka ili kumpata/kuwapata waliitenda tukio hili la kikatili.
"Tunatoa wito kwa vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi, kuanzisha uchunguzi wa kina na wa haraka juu ya tukio hili, kuhakikisha wahusika wanapatikana na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kukomesha vitendo vya aina hii.”
Aidha TLS imeeleza kuwa tukio hili linatengeneza hofu juu ya hali ya kiusalama ya mawakili na wataalam wa sheria nchini huku wakiiomba serikali kuhakikisha wataalam hao pamoja ma watetezi wa haki za binadamu wanakuwa salama.
Taarifa ya TLS iliyosainiwa na Rais wa chama hicho Boniface Mwabukusi imemtambua Wakili Masanja kama mwanachama mwenye namba ya uwakili 7664.
Moja ya kesi zilizompa umaarufu marehemu Wakili Masanja ni kesi ya shambulio la kimwili kwa kijana Hashim Ally iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul.
Source: Jambo TV