Tanganyika - Liemba

Tanganyika - Liemba

Kipala

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
3,763
Reaction score
700
Waheshimiwa, nina maswali mawili kuhusu ziwa Tanganyika na jina lake.

a) Yuko anayejua maana asilia ya neno "Tanganyika"?

Nilisikia ni TANGA (=la jahazi) + NYIKA (=pori).
Nina wasiwasi sana kwa sababu
# sielewi maana ya jina hili kama ni kweli
# sijaona habari ya uhakika kuwa jina lenyewe ni la Kiswahili - labda limetoka katika lugha nyingine na kuswahilishwa?

b) Je ni kweli "Liemba" ilikuwa jina la sehemu ya kusini ya ziwa Tanganyika kwa Kifipa?
Nilichungulia online kwa David Livingstone lakini sipati picha kamili - ama ni ziwa lenyewe au jina kwa eneo upande wa kusini wa ziwa au ni watu ?
 
Back
Top Bottom