Tanganyika na Zanzibar kutumia leseni za udereva tofauti

the horticulturist

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2012
Posts
1,959
Reaction score
1,907
Assallam Alleykum!
Poleni na majukumu ya kila siku. Mimi ni mtanzania mwenye leseni ya udereva ya Tanzania ila sasa niko kikazi Zanzibar (Unguja na Pemba) kazi itakayoniweka kwa zaidi ya miaka mitatu huku visiwani.
Kero yangu leseni yangu ya udereva huku haitumiki nimetafuta kibali cha kuendesha magari hivyo polisi akinisimamisha akiuliza leseni nampa leseni ya Tanzania na kibali cha kuendesha Zanzibar.
Swali langu kwanini kuna utofauti yaani kwanini leseni ya Tanzania haitumiki Zanzibar ilihali ni nchi moja?? Kibali inanibidi kila miezi mitatu nikate kingine na ni cha kulipia sio bure.

Naombeni ushauri wa kisheria kwanini leseni ya kuendesha magari ya Tanzania haikubaliki Zanzibar mpaka nikate kibali (driving permit) ambavyo naamini wanatakiwa wakate wageni ambao sio watanzania?
Kwanini uhalali wa leseni ya Tanzania haitumiki Zanzibar na kama sijakosea ya Zanzibar haitumiki bara?

Natanguliza shukrani
 
Aliekwambia ni Nchi moja ni nani wacheni kujitoa mshipa wa fahamu icho kitu mwakitamani sana ila hakitokua katu
Mna serikali yenu na sisi tuna yetu
Mna Raisi wenu tuna rais wetu
Mna mahakama zenu na sisi tuna zetu
Mna Bunge lenu nasi tuna letu
Mna wimbo wa taifa wenu tuna wetu
Bendera yenu nasi tuna yetu
Mnaanzaje kutwambia ni Nchi moja
 
Sarafu vipi mkuu?
 
Kiufupi sekta ya mawasiliano na uchukuzi sio jambo la Muungano. Kwa uelewa zaidi pitia katiba ujikumbushe mambo ya Muungano.
 
Okay ahsante sana ila hii inaumiza kwa sisi wafanyakazi maana tukiwa huku hatulipwi kama waajiliwa wa kimataifa
 
tanzania na zanzibar ni nchi mbili tofauti hakuna msada wa kisheria wala nini
 
Vipi jumuia ya Ulaya?
Hili swali limekushinda bora ukae kimya ulaya wana sarafu moja inayowasaidia katika uingiliano wa kibiashara within umoja wa ulaya lakini member countries wana safaru zao.
Sasa niambie kama Euro ni sarafu inayounganisha member countries za ulaya kwa case hii ya hapa inafananaje? Acha kutoa mifano ya kipuuzi.
 
Kama mada ni ya kipuuzi basi hata majibu na mifano nayo yatakuwa ni yakipuuzi.
 
Okay ahsante sana ila hii inaumiza kwa sisi wafanyakazi maana tukiwa huku hatulipwi kama waajiliwa wa kimataifa
Kuepuka gharama nenda kaombe leseni ya Zanzibar kwa kutumia hio leseni yako ya bara kuondoka na usumbufu wa kukata permit kila baada ya miezi mitatu. Mm nilifanya hivyo na nina leseni zote mbili. ( Hakuna msaada wa kisheria sababu huo ndio Muungano tuliinao kwa sasa)
 
Utaniita akjibu
Nikwambie hati ya Muungano ya waasisi haikuzidi mambo kumi na moja kilichoendelea ni kwamba Wadanganyika mkaendelea kuingeza mambo kadiri mtakavyo mkichukulia faida ya nyinyi kwa wengi bungeni mkadhharau hata sheria ya mambo ya muungano kupitiswa kwa Two third ya kura za wabunge wa Zanzibar mkajitia ubabaifu kupiga kura mambo ya muungano kwa Simple majority
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…