Tanganyika nchi yangu:

Tanganyika nchi yangu:

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
5,940
Reaction score
3,047
Kwa watanganyika wote ni muda muafaka kuanza mchakato wa KATIBA RASMI YA NCHI -REPUBLIC OF TANGANYIKA

Michezo hii ya wanasiasa wanaofaidika kwa Jasho ya Wavuja Jasho wa Tanganyika na kuwabebeshwa mizigo isiyoisha ufike muda na tuutue.

Hoja ya Kwanza Kikao cha Kwanza la Bunge la Tanganyika ni kujadili Ndoa hii ya Serikali Tatu na kutuletea Wananchi kupigilia msumari wa mwisho kwenye sanduku la Kura -(Demokrasia).

Wenzetu wamemaliza;

Kwa maoni yangu hakuna nia yoyote njema kwa wale wote wanaoshabikia serikali Tatu.

Na wale hakuna sababu yoyote ya kuwa na serikali tatu maana hakuna faida yoyote hasa kwa Watanganyika.

Kama hakuna uwezekano wa Serikali moja kwa sasa basi Serikali Mbili au Tatu haina maana yoyote na badala yake Kila Nchi Tanganyika na Zanzibar ziwe kivyake.Na ili kuwatendea haki wananchi na kuendeleza Amani basi kabla ya kuanza kwa Mchakato huu wa Katiba JMTZ unaoshabikiwa na Wanasiasa waliofilisika kimawazo ni bora wakaja na mpango wa upigaji kura ya -Serikali Moja ,Tatu au Mwisho wa Muungano.

Waswahili wana msemo usemao mkuje samaki angali mbichi .
Maana yake nini; Kwangu muda huu ni nzuri sana kwani tuko kwenye harakati na vuguvugu la kisiasa ,kijamii na kiuchumi na maamuzi yatakayopitishwa sasa yatatuweka miaka mingine 50 ijayo bila shida kwakuwa Idadi ya wengi wa vijana waliopo ndio wahusika wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Nchi hizi hivyo kuwashirikisha katika maamuzi ya aina ya Nchi na jamii tunayotaka waishi ni muhimu sana kuliko mawazo na mtazamo wa wanasiasa na aina ya utaalamu wa akina Warioba na Tume yake .

Sina tatizo na uzoefu wa Tume ya Jaji Warioba katika ufahamu wa masuala ya kisheria lakini kubwa ambalo Tume hii na wanasiasa wa Enzi hizo kinawasumbua ni kimvuli cha maisha waliyopitia na hivyo kimvuli hicho kinawakwamisha kutambua uhalisia wa sasa kuwa idadi kubwa ya Wakaazi wa Nchi hizi ni vijana waliozaliwa 1980s ambao kwao habari ya kumezwa kwa Zanzibar ,Ukomunisti na mambo mengineyo ya Enzi hizo kwao hayana nafasi na si muhimu.

Hivyo aina ya Nchi na mfumo wa utawala utakao tuhakikishia miaka mirefu ya Amani,Utengamano na Maendeleo ni kupitia baraka ya Kundi hili kwa kuwapa nafasi ya kujiamulia kupitia maoni na Sanduku la Kura na si kupitia kwa wanasiasa hawa wa Kidumu cha Chama Mapinduzi na Mapinduzi daima.

MODS;Naomba mwongozo wenu.

Tumekuwa na utamaduni wa kupiga kura ya Maoni kwa mambo kadhaa humu Jf.
Hivyo nilikuwa na pendekeza kuanzishwa kwa kura hiyo katika suala hili la Idadi ya Serikali ndani ya Jamhuri ya Tanzania kwa sasa.

Wangapi wanaunga ;
A.Serikali Moja
B.Serikali Mbili
C.Serikali Tatu
D;Sina Upande.
 
Hapa kama serkali3 ni gharama basi iwepo1 kama nayo moja haiwezekani muungano ufe!
 
Serikali moja tu,na sivinginevyo. Tuangalie kwa makini Kuna Watu wachache ambao wananufaika na uwepo wa serikali zaidi ya moja. Muungano tusiuvunje, bali tuudumishe kwakuwa na serikali moja tu .
 
MODS;Naomba mwongozo wenu.

Tumekuwa na utamaduni wa kupiga kura ya Maoni kwa mambo kadhaa humu Jf.
Hivyo nilikuwa na pendekeza kuanzishwa kwa kura hiyo katika suala hili la Idadi ya Serikali ndani ya Jamhuri ya Tanzania kwa sasa.

Wangapi wanaunga ;
A.Serikali Moja
B.Serikali Mbili
C.Serikali Tatu
D;Sina Upande.

cc Invisible
 
Last edited by a moderator:
Ni wakati sasa kwa Watanganyika kupima mambo.

Maelezo ya Warioba na Timu yake kuwa na Serikali Tatu eti ni kulinda Muungano hayana Ukweli hata kidogo na itakuwa suala la muda tu Muungano kuvunjika pale Tanganyika itakapo tangazwa upya.

Kwa maoni yangu na kwa jinsi hali ya mambo ilivyo-Kizazi cha Dot.com hakuna haja ya kuwapotezea watu muda na pesa nyingi. Rasimu ya Katiba inayopigiwa Chapuo na Ikulu na Timu ya Warioba haijaweka kinga yoyote dhidi ya kutovunjika kwa Muungano mara Serikali Tatu itakapoundwa kama vile Zanzibar ilivyojitangazia Katiba yake huku ikikiuka Katiba iliyopo
hivyo hivyo Tanganyika mbebaji mkubwa wa gharama hizi za kuendesha JM-Tanzania hakuna kinachomlazimisha kulipa/kugharamikia huduma kwa manufaa ya Nchi nyingine(Zanzibar).

Jibu la kutuondolea malalamiko yaliyopo kwa pande zote ni kuwa na Serikali moja ambayo kila Nchi inapoteza haki zake zote za awali na kujenga mazingira ya kuwa sawa kama kweli tuna nia ya kuwa na Afrika Moja- United States of Africa

... Noted:
- Serikali Moja
- Rais Mmoja
- Baraza la Mawaziri Moja
- Bunge Moja
- Jeshi Moja
- Katiba Moja
- Tanzania Moja
- nk, nk.
 
Back
Top Bottom