Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar?

Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar?

Clever505

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2020
Posts
1,183
Reaction score
2,256
Mimi naishi Zanzibar sasa ni mwaka wa 12, nimekuja huku nikiwa mdogo sana 2012 nikiwa na miaka 19, mpaka sasa naanza kuwa mtu mzima kuna mambo nayaona huku ambayo mtanganyika ukija huku ukakaa siku mbili/tatu huwezi kuyaelewa. Adui wakubwa wa Wazanzibar ni:

1. CCM
Huku watu wote hawaitaki kabisa ccm, hata ifanye mema gani hawaitaki tuuuu, cha kushangaza ccm inashinda uchaguzi. Hapo nafikiri inajulikana kinachofanywa na maccm kushinda.

2. Ukristo
Chuki dhidi ya ukristo ni kubwa sana huku ila we Mtanganyika ukija hapa kwa siku chache sio rahisi kuona hilo ila sisi ambao tunakutana na hawa watu kwenye mikusanyiko mbalimbali mfano, masokoni, kwenye usafiri wa umma, mahospitalini, kazini ndo tunajua jinsi ukristo unasemwa vibaya kila kona.

3. Muungano
Muungano unachukiwa na kila rika la mzanzibar ambaye tayari ameshaanza kujitambua, cha kushangaza sisi watanganyika tunaupambania sana. Huku watu wanafundishwa jinsi muungano unavyowabana, unavyowakosesha uhuru na nchi Yao, why watanganyika hatufundishwi faida yake kama kweli ipo?

Inawezekana kuna faida kiserikali lakini je, wananchi wa kawaida mitaani wanaelewa faida yake? Wanachi wa Zanzibar wanajua na wanahimizana kuukataa muungano wakidai unaifanya Zanzibar isiwe huru, vipi sisi watanganyika mbona hatuna chochote cha kukizungumza mtaani ambacho ni kizuri kitakachotushawishi wananchi wa kawaida tuupambanie?

Huwezi kukuta vijana wa kitanganyika mtaani wanazungumzia uzuri wa muungano lakini ni mara nyingi sana mimi naona vijana wa kizanzibar wamekaa vijiweni wanauponda muungano na hawautaki kabisa.

Kama muungano ni mzuri tuelezeni tujue ili tuwe proud nao na tuupambanie kufanya uwe imara ila kama hamfanyi hivyo mnatufanya tusiwe na la kusema hata tunapokuta watu wanauponda. Hapa nilipo mi nipo tayari kwa chochote kwamba tuuvunje au tuendelee kwa sababu sioni faida yake kwangu ila kijana wa kizenji yeye jibu ni moja tu kwamba "hatuutaki muungano"

Kwa akili yangu huwa nawaza na kujisemea kwamba Nyerere alikuwa na wazo zuri la kutengeneza muungano ila alishindwa kabisa kuutengeneza muungano bora. Kwanza aliua jina la Tanganyika na kuliacha Zanzibar, hapo maana yake ni kwamba alitengeneza uzanzibar na utanzania wakati ilibidi atengeneze kitu kimoja tu utanzania. Pili, kufanya wazanzibar wawe huru kutawala hadi Tanganyika ila watanganyika hawana uhuru wa kutawala Zanzibar hilo ni kosa kubwa.

Kwa sasa tuna Tanzania na Zanzibar na wala si Tanganyika na Zanzibar hili ni kosa la Nyerere. Watanganyika tunalitaka sana jina la Tanzania ila wazenji hawataki kabisa kujihusisha nalo.

Wazee, tufundisheni faida ya muungano ili na sisi tufundishe vizazi vyetu, mnapoendelea kukaa kimya wasioutaka muungano hata kama ni wachache watashinda kwa hoja maana wanaoutaka muungano hawana points za msingi. Mimi hapa nilipo sina chochote cha maana cha kuja kuwafundisha kizazi changu kuhusu umuhimu wa muungano ila kijana wa kizanzibar anayo mengi ya kumueleza mwanae ili auchukie muungano.


ZAIDI UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
= > Lipo wapi tatizo kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Tafakari!

= > Waliohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wafikia hatua gani?

= > Yajue mambo 22 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

= > Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar?

= > Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

= > Fahamu A-Z kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

= > Tuna Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tu, siyo Tanzania
 
Wazanzibari walio wengi ni wanafiki, ni wachoyo, ni wabinfsi, ni wavivu, ni wanyonyaji, wanapenda kudeka kama watoto wadogo, wanapenda kulalamika hovyo!

Kiufupi huu Muungano ni wa kinyonyaji! Hivyo uvunjike tu ili kila nchi ijitegemee kivyake.
 
Wazee, tufundisheni faida ya muungano ili na sisi tufundishe vizazi vyetu, mnapoendelea kukaa kimya wasioutaka muungano hata kama ni wachache watashinda kwa hoja maana wanaoutaka muungano hawana points za msingi. Mimi hapa nilipo sina chochote cha maana cha kuja kuwafundisha kizazi changu kuhusu umuhimu wa muungano ila kijana wa kizanzibar anayo mengi ya kumueleza mwanae ili auchukie muungano.
Umesema kwenye kichwa cha mada yako kwamba:"Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar", lakini ndani ya mada, unayoyaongelea ni tofauti na lengo hilo.

Kwanza nikupe pole, kuishi katika hali ngumu namna hiyo miaka yote hii. Sijui shughuli inayokufanya ubaki huko katika mazingira hayo uliyo yaeleza, ambayo naona kuwa ni magumu sana. Kura huwezi kupiga kumchagua kiongozi yeyote unayemtaka, na kama wewe dini yako ni tofauti na hao walio wengi, wewe ni kama mtu wa gredi ya chini kuliko wengine wote.

Hapana, usimlaumu Nyerere kwa hiyo hali ya muungano ilivyo. Muungano haukuwa kamili ulipo anzishwa. Kulikuwa na hatua za ziada kuendelea kuwaweka karibu zaidi raia wa pande zote mbili. Badala ya kufuata lengo hilo lililokusudiwa toka mwanzo, viongozi waliofuata (CCM) wakageuza lengo hilo na kufanya kila juhudi kutafuta njia za kuwafurahisha waZanzibari, kwa kuwapa rushwa kwa njia mbalimbali waZanzibari kupitia kwenye "Kero za Muungano" ambazo zilikuwa kila mara zinaibuliwa toka Zanzibar, zikiratibiwa na kundi ambalo tokea mwanzo kabisa hawakuupenda muungano.
Kwa sasa hivi, kundi hilo ndilo linalotawala, siyo Zanzibar pekee, bali hata huku kwenye serikali ya muungano; kinara wake akiwa Samia.
Nisiandike mengi, lakini inatosha kumalizia kwa kusema kwamba endapo Samia hataumaliza kabisa muungano huu, basi hapo kutakuwa na muujiza wa kipekee sana kwa Tanzania.
 
Mtu ajitolee kwenda kuchambua ule mchanga kwenye kibuyu uliochanganywa kipindi cha muungano. Mchanga mmoja mmoja. Upande huu mchanga wa tanganyika, upande ule wa visiwani urudishwe kila kwenye sehemu inayomuhusu
 
Umesema kwenye kichwa cha mada yako kwamba:"Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar", lakini ndani ya mada, unayoyaongelea ni tofauti na lengo hilo.

ba endapo Samia hataumaliza kabisa muungano huu, basi hapo kutakuwa na muujiza wa kipekee sana kwa Tanzania.
Nimeyaanza hayo mengine kuonyesha vile wazenji hawapendi kabisa mambo ya kutoka bara, ingekuwa ni maamuzi yao wasingeruhusu kabisa hayo mambo niliyoandika. Naendelea kumlaumu Nyerere kwa sababu yeye ndo mwanzilishi wa huu muungano ambao hadi anaondoka duniani alishindwa kuuweka sawa.
 
Back
Top Bottom