Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar?

Tanganyika ni lazima iendelee kuungana na Zanzibar?

Watu 10000 kama wewe wanatakiwa TANGANYIKA huenda TANGANYIKA yetu ikarudi!
Wao hawaitaki Tanzania tunawalazimisha tu, kama kuna faida ya kuulinda huu muungano kwa sisi watanganyika tuambiwe tujue. Kama vipi kila mtu abaki na nchi yake
 
Mtu ajitolee kwenda kuchambua ule mchanga kwenye kibuyu uliochanganywa kipindi cha muungano. Mchanga mmoja mmoja. Upande huu mchanga wa tanganyika, upande ule wa visiwani urudishwe kila kwenye sehemu inayomuhusu
Kwani huu ni muungano wa mchanga Ndugu mpaka tudeal na michanga
 
Mkuu mbona kwa mujibu wa Jina lako hapo juu, muungano wa ndoa yako unaulinda hadi hata baada ya kifo, ila muungano wa JMT unashabikia uvunjike???

Tukueleweje???

Ama kweli za kuambiwa changanya na zako. Tumekusoma!!!
Kwahiyo muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni mke na Mme?
Nani mwanamke kati yake?
 
Baada ya Samia kuingia madarakani anaijenga zenji kila sehemu, we hujasikia hadi rais mwinyi anaitwa "rais mabati" kwa sababu kila kona ya zenji kuna fensi la mabati ikiashiria kuna ujenzi ndani yake.
Na huo ujenzi mwingi Zenji unafanywa kwa kutumia fedha zanazochotwa Tanganyika
 
Barabara mpya ya 2020 eti inakwanguliwa na kujengwa tena upya we unafikiri hii ni jeuri ya nani kama si Samia?
Kufuru hiyo.
Pesa ya Tanganyika haina mtetezi wala mlinzi.
Halafu upande wa Tanganyika kuna baadhi ya shule za vijijini huko wanafunzi wanakaa chini
 
Kufuru hiyo.
Pesa ya Tanganyika haina mtetezi wala mlinzi.
Halafu upande wa Tanganyika kuna baadhi ya shule za vijijini huko wanafunzi wanakaa chini
Ccm Haina mpango kabisa wa kujenga Tanzania ila Samia ana mpango wa kujenga Zanzibar. Huku shule zote zinajengwa vizuri kinoma tena maghorofa.

Kuna sehemu ambapo hadi roho iliniuma nikajiwazia kwamba watu hawana kabisa huruma na pesa za uma, wametumia pesa nyingi kujenga kituo cha daladala, sasa kipo mbali kidogo na mjini eti watu washuke hapo then watembee hadi mjini. Watu wakagoma, kilichofanyika ni kwamba wamevunja then wanajenga ghorofa kubwa sijajua ni soko ama vipi. Yaani kituo hakijatumika hata mwezi mmoja wamekivunja.
 
Back
Top Bottom