Wao hawaitaki Tanzania tunawalazimisha tu, kama kuna faida ya kuulinda huu muungano kwa sisi watanganyika tuambiwe tujue. Kama vipi kila mtu abaki na nchi yakeWatu 10000 kama wewe wanatakiwa TANGANYIKA huenda TANGANYIKA yetu ikarudi!
Kwani huu ni muungano wa mchanga Ndugu mpaka tudeal na michangaMtu ajitolee kwenda kuchambua ule mchanga kwenye kibuyu uliochanganywa kipindi cha muungano. Mchanga mmoja mmoja. Upande huu mchanga wa tanganyika, upande ule wa visiwani urudishwe kila kwenye sehemu inayomuhusu
Ni suala gani duniani limeishawahi kuwa sawa?Kwa hiyo we huu muungano unauona upo sawa?
Naona unataka tubishane tu, ushahidi gani unautaka! Mi naongea ninachokiona,
Kwahiyo muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni mke na Mme?Mkuu mbona kwa mujibu wa Jina lako hapo juu, muungano wa ndoa yako unaulinda hadi hata baada ya kifo, ila muungano wa JMT unashabikia uvunjike???
Tukueleweje???
Ama kweli za kuambiwa changanya na zako. Tumekusoma!!!
Anaijenga sana zenji tena saaaana, kama magufuli alivyokuwa anaijenga chato
Na huo ujenzi mwingi Zenji unafanywa kwa kutumia fedha zanazochotwa TanganyikaBaada ya Samia kuingia madarakani anaijenga zenji kila sehemu, we hujasikia hadi rais mwinyi anaitwa "rais mabati" kwa sababu kila kona ya zenji kuna fensi la mabati ikiashiria kuna ujenzi ndani yake.
Kufuru hiyo.Barabara mpya ya 2020 eti inakwanguliwa na kujengwa tena upya we unafikiri hii ni jeuri ya nani kama si Samia?
Ccm Haina mpango kabisa wa kujenga Tanzania ila Samia ana mpango wa kujenga Zanzibar. Huku shule zote zinajengwa vizuri kinoma tena maghorofa.Kufuru hiyo.
Pesa ya Tanganyika haina mtetezi wala mlinzi.
Halafu upande wa Tanganyika kuna baadhi ya shule za vijijini huko wanafunzi wanakaa chini