Tanganyika ni nchi inayotumikishwa kwa kivuli cha Tanzania?

Juzi tu siku ya uhuru wa Tanganyika nikashangaa sana kuona bango miaka 62 ya uhuru. Nikajiuliza kwa nini mwandishi hakutaka kuandika neno Tanganyika mpaka leo sielewi

Mara utaona uhuru wa Tanzania bara sijui ndio nchi gani
Ninakereka sana ninapolisikia hilo jina, Tanzania Bara.
 
Je uliwahi kuona wanaogopa kutaja jina la majimbo yao mfano Washington, Newyork
Wataogoopaje wakati Marekani ni moja yenye majimbo zaidi ya hamsini? Na huo Muungano haupo kwa maslahi ya watawala kama ulivyo wa Tanganyika na Zanzibar, ni kwa manufaa ya wananchi.

Ndiyo maana pamoja na ukubwa wote wa Marekani, husikii kero kama za Watanganyika na Wazanzibar. Na sisi tungekuwa na Muungano kama huo usingesikia manung'uniko yoyote.

Lakini kwa huu uliopo, Wazalendo hawatakaa wauvumilie huo udhalimu wa watawala.
 
Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Udhalimu hautatawala siku zote.
 
Huo ubaguzi kaufanye ndani ya ukoo wenu. Marekani ni muungano wa nchi 50 na wanaona fahari sasa wewe nyani unaongea nini

Marekani Kuna nchi ndani ya nchi? Kule Kuna states wakati hapa ccm hamtaki sera za majimbo.
 

Muungano ambao mbara hawezi kuwa kiongozi ama kumiliki ardhi Zanzibar, lakini mzanzibar anaweza kupata chochote huku bara?! Huo sio muungano Bali ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Ukitaka kuhakiki maneno yako nenda Sasa hivi Zanzibar uone kwa macho yako maendeleo yaliyofanyika mara baada ya kifo cha Magufuli. Hapo ndipo utaona utamu wa muungano kwa Zanzibar
 
Ukitaka kuhakiki maneno yako nenda Sasa hivi Zanzibar uone kwa macho yako maendeleo yaliyofanyika mara baada ya kifo cha Magufuli. Hapo ndipo utaona utamu wa muungano kwa Zanzibar
Na huo ni utangulizi tu. Fedha za bandari za Tanganyika zitakapoanza kuingia ndipo maendeleo yatakapoanza rasmi.
 
Marekani Kuna nchi ndani ya nchi? Kule Kuna states wakati hapa ccm hamtaki sera za majimbo.
Fatilia vizuri mitandao ya kijamii nini kinaendelea texes uko marekani,na kenya pia km mmezowea kudanganywa na wana siasa wkutumien ukimaliza uchaguz wapeleke vimada vyao bungeni endelea tu kudanganywa usifanye kazi kwa bidii hubiri majimbo katiba mpya na ratiba ya maandamano
 

Hatufanyi kazi, umewahi kuona mtu anakuletea familia yake uilishe we mtumwa wa ajira?
 
Wewe unaunga mkono Zanzibar kuitumikisha Tanganyika?
 
Hatufanyi kazi, umewahi kuona mtu anakuletea familia yake uilishe we mtumwa wa ajira?
Hata kuitetea nchi yetu ya Tanganyika ni kazi pia, sema hii ni ya kujitolea.
 
Kweli tofauti 'na wenzao wa zanzibar hata kipindi cha karume wengelikataa kamanda wengeshirikishwa kutoa maoni
 
Nimezaliwa ndani ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar miaka yote naijua Zanzibar yenye utamaduni wake pamoja na sheria mbalimbali pamoja na siku yake iliopata uhuru (mapinduzi day) sina maana kwamba muungano hauna maana hapana najaribu kuzua hoja kwamba kuna mahali waasisi wa Tanganyika walikosea , hakuna historia ya Tanganyika maana ata siku ya uhuru wake kama taifa inafahamika kama uhuru wa Tanzania wakati hii Tanzania ni taifa la Muungano ambalo halikutawaliwa na wala halikupata uhuru. Iko wapi Tanganyika!!?
 
Mapibduzi sio siku ya uhuru wa Zanzibar.
 
Mapibduzi sio siku ya uhuru wa Zanzibar.
Hoja yaje yake ya Msingi ni kwa nini Tanganyika na historia yake yote imefunikwa na Tanzania? Kwa nini Tanganyika isienziwe na kawa ifanyikavyo kwa Zanzibar?

Iko wapi Tanganyika??
 
HATA VIONGOZI HAWAJUI NYERERE ALIIFICHA WAPI NDIO WANASEMA UHURU WA TANZANIA BARA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…