Tanganyika packers

Tanganyika Packers hapo Kawe ilishauzwa na PSRC kwa mwarabu mmoja toka mashariki ya kati; Adamjee alikuwa dalali tu. Mauzo ya kiwanda hiki yalipitishwa na waziri mkuu mstaafu Sumaye!! Kwahiyo kile kibabu cha Kawe club kinajidanganya tu siku ya siku wenyewe wakija itabidi waondoke; waarabu walilipa mamilioni ya shilingi. Taarifa za usahihi nadhani zipo Consolidated Holdings .
 
Tanzania, nakupenda kwa moyo wangu wote.........!
 

Unaweza kutusaidia bei yake na dalali alichukua ngapi?Maana dalali huyu alizungusha ukuta ambao sasa unaanguka!Nakumbuka Mama yetu Rwakatare nae alikuwamo pia.
 
Tanzania, nakupenda kwa moyo wangu wote.........!

Moyo usiodunda, ungekuwa unadunda usigeipenda Tanzania.

Walioipenda Tanzania kwa moyo wote hawawezi kuwa hai, the Sokoines, Nyereres, Kawawas etc. Orodha ni fupi wako wachache sana.
 
Rta Mlaki anajuwa zaidi kuliko yoyote kuhusu hiyo tanganyika packers, nijuavyo kuna mstaafu wa hapo tanganyika packers amewahi kufungwa kisha kachomoa bati la uzio kwa hasira.
 
Hii mada nimeifungua haraka haraka nikitegemea majibu ya maana! Ila naona hakuna aliyetoa ufafanunuzi wa kueleweka kuhusu hili eneo la kiwanda. Ni eneo kubwa mno na lina beach plots pia. Yaani nahisi mafisadi huwa wanapatolea macho mno ndio maana hata hapauziki.

Yule babu wa Kawe Club niliambiwa alikuwa Operations Officer wa kiwanda hicho enzi hizo. Ameng'ang'ania ile Club kwa kuwa hawajalipwa mafao yako mpaka leo.
 

Sijakupata mkuu...nadhani niliianzisha mimi.....its alright though hata mimi nataka kujua what next na eneo lile...naikumbuka sana ile beef yao ya kopo ikiitwa LEENOX.....halafu kulikuwa na wale CHAKULA BARAFU(NATIONAL COLD CHAIN OPERATIONS-NCCO) walikuwa wanatengeneza khima(minced meet but uncanned)...
 
Safari , umenikumbushia Ufahari wetu, kwanini tumerudi nyuma ?
hivi tungeendelea na kasi ile ile ya uzalishaji kuanzia Tanganyika packers, UFI, Viwanda vya Nguo, Maturubai, tungekua wapi leo....bado najiuliza ni wapi tunajikwaa.
 

Mkuu,

Sikumaanisha kwamba mada nimeianzisha mimi, nimemaanisha kwamba nimeifungua ili kuisoma!
 
I live in Kawe every day I pass there and feel as crying. kweli eneo ni kubwa na liko sehemu nzuri zaidi naona karibu yake kuna dampo na ukipita ni harufu kali na zaidi kuna watu wanacheza mpira pia timu kama Simba, Azam wanaenda kufanya mazoezi.Kuna viwanja zaidi ya vitatu vya mpira wa miguu. Government should do something
 
Safari , umenikumbushia Ufahari wetu, kwanini tumerudi nyuma ?
hivi tungeendelea na kasi ile ile ya uzalishaji kuanzia Tanganyika packers, UFI, Viwanda vya Nguo, Maturubai, tungekua wapi leo....bado najiuliza ni wapi tunajikwaa.

Amazingly we had 400 parastatals ante-PSRC....lakini tukauza hata best performers at losses na viwanda vingine vikafungwa kabisa.....post-PSRC hatujajenga hata kimoja!!!!....na wale NDC sijui wnafanya nini...nchi zingine taasisi ya umma ikitaka kuuzawa inpelekwa kwenye stock/capital markets sisi tuna mfumo wa ajabu kabisa...watanzania wana uwezo kabisa wa kununua hisa za taasisi hizi lakini sisi lazima tuuze nje...imagine ATC wakiuza hisa zao DSE through IPO response itakuwaje....JUST angalieni KQ hapo kwa jirani....lakini sisi porojo tupu ati SONANGOL ya China ndio muwekezaji...mimi najua SONANGOL ni waangola
 
INATIA hASIRA, WAKATI WA MIAKA YA 1961 HADI MIAKA YA 80, nnchi hii ilikua inakwenda kasi katika uzalishaji, wakati huo hatukua na wasomi wakutosha,nyenzo na wala watu kama raslimali haikua kubwa.
leo ambapo nnchi inazalisha wasomi mamia kwa maelfu, mwaka baada ya mwaka, ndicho kipindi ambacho sekta ya uzalishaji Viwandani na mashambani imeeanguka zaidi, Je elimu yetu haijatusaidia kutu.
 

Mbaya zaidi watoto wa wafanya maamuzi wetu wanasoma nje,wakimaliza wanafanya kazi nje,wakikwama baba zao wanawakopea ubalozini halafu hawalipi ila wakifa ndio wanarudishwa nyumbani kwa mbwembwe nyingi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…