Tanganyika packers

Unaweza kutusaidia bei yake na dalali alichukua ngapi?Maana dalali huyu alizungusha ukuta ambao sasa unaanguka!Nakumbuka Mama yetu Rwakatare nae alikuwamo pia.

Adamjee alitaka kuwatapeli hawa waarabu kwa kukikata kile kiwanja ili achukue ile sehemu ya juu aliozungushia ukuta na kuwabakizia hawa waarabu sehemu ya kwenda baharini na ndio maana alizungushia ukuta. Waarabu hawa wana lawyer wao anaeangalia maslahi yao na wamekwisha tengeneza michoro ya nini wanataka kulifanyia hili eneo. Kama nilivyosema awali habari zote za hili eneo ziko Consolidated Holding Corporation. Halima Mdee mbunge wa Chadema alipeleka swali bungeni juu ya matumizi ya eneo hili sijui alijibiwa nini!!
 

Hii CHC inawajibika kwa nani? Mh.Mdee kama ni member tudokeze please....
 

Mheshimiwa nchi inazalisha wasomi lakini wenye kufanya maamuzi nchi hii siyo wasomi bali ni walewale makasuku wa CCM tangu enzi za chama kimoja.
 
Kwa nini kijengwe Dar wakati hakuna hao wanyama wa kuwasindika?
Kwani ile Songas ya ubungo inatoa ges wapi?Hatuangalii tu mali ghafi lakini pia soko, nishati, miundombinu,labor, (Nadhani bandari, diesel, umeme,na hata soko zote ziko dar)
 
Kwani ile Songas ya ubungo inatoa ges wapi?Hatuangalii tu mali ghafi lakini pia soko, nishati, miundombinu,labor, (Nadhani bandari, diesel, umeme,na hata soko zote ziko dar)

Songas ilishauriwa ijengwe Kilwa wakubwa wakapindisha.Wakati TPL inajengwa ilikuwa nje ya mji sasa ni tofauti.
 

Kweli kabisa NM, Tanzania kama kweli tuko siriazi twaitaji viwanda vingi kama hivyo na si kuwa taifa la wachuuzi tena bahati mbaya uchuuzi wa bidhaa feki za kichina, maana ndo zimeyajaza maduka yetu hivi leo, hatuna viwanda si vya nguo, pipi, matunda wala viatu NK.

Ukienda Kariakoo utashangaa, kuna shati DISPOZABO toka china kwa shs 500/- tu, na maduka kila kona lakini hakuna hata kitu kimoja kinachotengenezwa Bongo.

Tumebakia taifa la vitu feki na mitumba tu, maana sasa hivi kila kitu anachotumia mbongo kama si mchina basi ni mtumba period!

Inasikitisha sana tena sana hali hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…