Tanganyika (Tanzania) Ingekuaje kama Wajerumani wangeshinda WW II

Katika jumuiya yote ya ulaya hakuna majitu katili kama wajerumani, hadi leo. Kwa hiyo kuwepo kwao kwetu mda mrefu kungetuongezea machungu. Weeeeeee, wale jama achana nao.
Shukuru tu haya maingereza yaliyaondoa.
 
Katika jumuiya yote ya ulaya hakuna majitu katili kama wajerumani, hadi leo. Kwa hiyo kuwepo kwao kwetu mda mrefu kungetuongezea machungu. Weeeeeee, wale jama achana nao.
Shukuru tu haya maingereza yaliyaondoa.
Waingereza na Wajerumani wenyewe hawapatani asilani, mwingereza ni mnafiki lakini anahuruma.
 


Nchi yetu ilipewa Uingereza baada ya vita ya 1 na siyo ya 2 hivyo wkt wa vita ya 2 tulikuwa hatuna uhusiano na Ujerumani tena!
 
Walishinda ya kwanza na kushindwa ya pili mkuu. Ndiyo mwingereza alikuja huku kwetu.
Nadhani tatizo lako lipo hapa.

Ukweli ni kwamba Wajerumani wakishawapata vita ya kwanza ya Dunia (1914-1918) na ndipo wakanyang'anywa makoloni yao ya Deutscheostafrika (yaani eneo love la Tanzania bara, Rwanda na Burundi), Namibia (kusini mwa Afrika) pamoja na Togo na Kamerun huko Afrika ya Magharibi. Katika vita ya pili ya dunia Wajerumani walipigwa kwa mara ya pili.

Tafadhali tembelea vyanzo vyako kwa mara nyingine.
 
Asante mkuu lakini tulishaliweka hili sawa na mkuu Barbarosa.
 
Makoloni ya Mjerumani Afrika ilikua Tanganyika na Namibia,
Deutsche Ost Afrika(German East Africa) ni Nchi tatu Tanganyika, Rwanda na Urundi(Burundi), Makoloni mengine yalikuwa ni Namibia(Deutsche Süd West Afrika); Kamerun na Togo.

Walishinda ya kwanza na kushindwa ya pili mkuu. Ndiyo mwingereza alikuja huku kwetu.

Mwingereza hakuja tu kwa hiari au kwa kushinda vita bali, alikabidhiwa Tanganyika na Umoja wa Mataifa( League of Nation) aisimamie kama baba mlezi mpaka itakapokuwa na uwezo wa Kujitawala.
Rwanda na Urundi alikabidhiwa Ubelgiji(Ubeleji) , Togo na Kamerun alikabidhiwa Ufaransa.
Ujerumani akaachiwa Namibia pekee.
 
Asante nilifahamu kukabidhiwa nchi kwa Mwingereza na ndiyo maana Nyerere alikwenda UN kueleza kuwa tukotayari kujitawala.
 
Pia ninaona kwa muda aliokaa Mwingereza kama mkoloni hakutenda mengi kwani alijua yeye ni mdhamini tu, nguvu yake nyingi aliielekeza Kenya.
 
Samahani kidogo ni vita vya kwanza vya dunia kati ya 1914 na 1918.
 
Makaburu ni mchanganyiko Wa waholanz(dutch),wafaransa waliokimbia mateso ya wafalme(haguenotes) na wajeruman wachache.wajeruman siyo wa Dutch,nchi yao wao wanaiita Deutch tamka dochi,Waswahili wakawaita wa dutch.hivyo tujaribu kutofautisha ili kuweka kumbukumbu sahihi.
?
 
 
Walishinda ya kwanza na kushindwa ya pili mkuu. Ndiyo mwingereza alikuja huku kwetu.
Do not falsefy historical fact,wajeruman walishindwa vita zote mbili ww1 na ww2.Ww1 ndiyo iliyowafanya wakapoteza makoloni yote Africa na hivyo vita ilipiganwa sehemu mbalimbali za Africa,kwa Ww2 vta kias kikubwa haikupiganiwa Africa kwa sababu ukiondoa Ethiopia na Africa kaskazin kwa Muitaliano mataifa ya Axis hayakuwa na makoloni.Ww2 ilikuja kama njia ya Ujeruman kurejesha makoloni aliyopoteza wakati was ww1 pamoja na mambo mengine
 
Ukweli ni kwamba,kwasababu tulishaingia kwenye maisha yao,mjeruman angetufaa sana maana hili lilikuwa ni kolon lake hivyo angepora raslimali nyingi lakini pia angeacha infrastructures nyingi Sana kunuondoa ingesumbua SNA na siasa ya ujamaa huenda isingesomeka katika historian yetu.
 
Historia inaonesha Tanganyika ilitwaliwa na Uingereza baada ya Ujerumani kushindwa WW I(1914-1918). Wakati wa vita vya WW II, tayari mjerumani alikwishapoteza makoloni yake siku nyingi.
Mjerumani alipokonywa makoloni mnamo mwaka 1919 kama adhabu ya kumpunguza nguvu ili asiweze kusababisha vita tena , baada ya mkutano wa usuluhishi wa Versailles, nchini Ufaransa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…