Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wananchi wa vijiji vya Bungwe, vikonge, Ngomalusambo katika kata ya Tongwe wilayani Tanganyika katika mkoa wa katavi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali na kubwa zaidi ni kokosekana kwa zahanati katika vijiji vyao,.
Wanakijiji wa kutoka kijiji cha Bungwe wamekuwa wakisafiri umbali wa kilomita zaidi ya 50 kufuata huduma za Afya katika kijiji cha Majalila kilichopo katika kata hiyo ya Tongwe.
Ally mashaka ambae ni Mwenyekiti wa kijiji cha Majalila amesema kuwa wanakijiji kutoka vijiji jirani hulazimika kulipa boda boda elf 20 na elfu kumi ya mafuta ya pikipiki na hivyo kufanya jumla ya usafiri ni elfu 30. Kufuata huduma za Afya katika kijiji chake ambacho ndio chenye zahanati na kituo cha afya ambavyo vyote havina huduma ya kulaza wagonjwa wala kuwekewa damu.
Kukosekana kwa zahanati katika hivyo pamoja na gharama usafiri zimesababisha wanawake wengi kujifungulia majumbani jambo ambalo ni hatari kwa uhai wao na hata wakati mwingine husababisha vifo
Mbali na Kukosekana kwa zahanati katika vijiji hivyo pia ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwani visima walivyojengewa na wahisani vingi vimeharibika na havifanyi kazi hivyo basi hutumia maji ya. Mito pamoja na mifugo ambayo sio salama kwa afya zao.
Miundombinu ya barabara pia ni tatizo katika kata hiyo kwani barabara zenyewe ni mbovu na hazijachongwa.