Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
NATAMANI KUFUKUWA MAKABURI - part X
Maalim Salim Kombo Saleh (ZPPP) Mbunge wa Jimbo la Tumbe, Pemba katika serikali ya uhuru alikuwa waziri wa sheria na mambo ya ndani wa Zanzibar.
Mwaka 1994 alinieleza kuwa siku ya tano baada ya mapinduzi walikabidhiwa kwa Mkuu wa Gereza la Dodoma, Tanganyika:
"Nilikuwa na wezangu wawili tuliopelekwa Dodoma, Abadhar na Dk Baalawy."
Anasema: "Tulisafirishwa kutoka Zanzibar, Siku ya Jamanne, Januari 14, 1964 tulipofika Dar es Salaam tukagawanywa kwenye magereza tofauti ya Tanganyika."
Anasema siku ya pili yaani Jumatano, Januari 15 walipelekwa Dodoma. Walikaa kwenye gereza hilo hadi mwaka 1968 Nyerere alipowaachia huru.
Lakini, anasema kuachiwa kwao huru Karume haikumfurahisha, walikamtwa tena na askari kutoka Zanzibar.
Anasema: "Dodoma ndiyo gereza kuu kwa Tanganyika, lenye zana za kunyonga wahalifu wanao hukumiwa adhabu ya kifo au vifungo vya maisha na muda mrefu."
Anasema: "Mawaziri wote wa Serikali ya huru ya Zanzibar, hatukupelekwa mahakamani kwa maana hatukuwa wafungwa tulikuwa 'detention' (kizuizini) kwa miaka yote kumi."
Alinieleza, muhalifu awe amehukumiwa adhabu ya kifo kwenye mahakama za Arusha, Lindi, Dar es Salaam, Morogoro au Mbeya au Kigoma au popote Tanganyika, hukumu yake inatekelezwa kwenye Gereza la Dodoma:
Anasema: "Zana yaani, vitendea kazi vya kunyongea wahalifu wanaohukumiwa adhabu ya vifo vipo 'Dodoma Central Prison' (Gereza Kuu Dodoma)."
Maalim Salim Komba, alinieleza kuwa Sk Mohamed Shamte, Waziri Mkuu wa Serikali Huru ya Zanzibar, alifungwa kwenye Gereza la Mtwara. Wenzao wengine walifungwa Singida, Tabora na Tanga.
Awali katika makala zilizopita nimeeleza kuwa mawaziri wa serikali ya uhuru ya Zanzibar niliyopata kukutana nao ni pamoja na Maalim Salim Kombo.
Serikali ya uhuru ya siku 33, ilipoangushwa Januari 12, 1964 alifungwa kwenye Gereza la Dodoma, Tanganyika.
Mawaziri wengine waliyofungwa gereza hilo, ni pamoja na Abadhar Juma Khatib (ZPPP) aliyekuwa waziri wa kilimo na Dr Ahmed Edarus Baalawy (ZNP) waziri wa afya, ustawi, mawasiliano na kazi, wote wa serikali ya uhuru.
Sk Mohamed Shamte Hamad (ZPPP), Waziri Mkuu wa Zanzibar na Sk Omar Hamad Mussa Mkamandume (ZPPP) waziri mdogo wa kilimo wa serikali ya uhuru wote walifungwa Mtwara.
Sk Mohamed Shamte, alikuwa mbunge wa ZPPP wa Jimbo la Chambani huku, Sk Omar Mkamandume alikuwa Mbunge wa ZPPP wa Jimbo la Mtambile, Pemba amlimshinda Malik Haji wa ASP.
Makala zilizopita nimeeleza kuwa makubaliano ya kuunda serikali yaliyofikiwa baina ya vyama vya ZNP na ZPPP, ilikuwa ni ZPPP cha Sk Mohamed Shamte, kitakuwa na waziri mkuu, mawaziri wawili na naibu waziri mmoja.
Ilifanyika hivyo, Waziri Mkuu Sk Mohamed Shamte, Mawaziri ni Abadhar Juma (Kilimo) na Maalim Salim Kombo (Sheria) na Sk Omar Hamad Mkamandume (Naibu Waziri wa Kilimo), wote wa ZPPP.
Nafafanua kidogo; Maalim Salim Komba, alinieleza kuwa mwaka 1968 baada ya miaka minne kukaa gerezani, Nyerere (Julius), aliwaachia huru yeye (Salim Kombo), Dr Balawy na Abadhar.
Anasema, siku ya tatu baada ya kuachiwa wakiwa Dar es Salaam, Karume (Abeid Amani) alipopata habari kuwa kuna baadhi ya mawaziri wa zamani wameachiwa, alituma watu kwenda kuwakamata.
Alinieleza, kuanzia mwaka 1968 walikaa Gereza la Kiinuamiguu, Unguja kwa Bamkwe, hadi mwaka 1974 Mzee Aboud Jumbe, alipowaachia huru kufuatia msamaha wa wafungwa katika sherehe za mapinduzi za miaka kumi. Mzee Karume, hapo keshauawa.
Anasema: "Baada ya sherehe kumalizika Jumbe (Aboud), alitushauri tufanye kazi mimi nilipelekwa Idara ya Elimu Vuga, karibu na mahakama kuu," alisema na kuendelea.
"Abadhar alikwenda zake Pemba, Wete kwao alirudi kwenye shirika la ZSTC la kuuzia karafuu na umri wake ukawa mfupi akafikwa na faradhi ya mauti."
"Dr Baalawy, watoto wake wa Dubai walimchukuwa kwenda kuishi naye Dubai na Sk Mohamed Shamte alibakia Dar es Salaam kwa mke wake Bi Maida Issa Sharif hadi alipoondoka Duniani.
Lakini anasema: "Mwaka 1969 na 1970 Nyerere, aliwapa ushauri wenzetu walokuwa wamebaki kwenye magereza ya Tanganyika, kuwa yuko tayari kuwaachia lakini waondoke nchini kama wanapo pakwenda."
Anasema: "Baada ya hapo wengine waliondoka kabla ya kufikisha miaka 10 akina Ali Muhsin Barwani, Maulid Mshangama na wengine."
"Sk Mohamed Shamte, Juma Aley na Mkamandume walikaa gereza hadi walipomaliza miaka kumi hawakutaka kwenda kuishi nje."
Anasema: "Nyerere hakutaka yatokee kama yaliyotokea kwetu alituachia huru lakini, Karume aliamua kutukamata tena, hakuridhishwa na uamuzi wa Nyerere."
Anasema: "Picha baina ya Nyerere na Karume, ilionekana kuwa hawana masikilizano mema. Ni Ishara kuwa walikuwa hawana maelewao."
Narudi nyuma; Mzee Karume aliwashawishi wananchi wa Zanzibar, kuwa na mwingiliano wa damu kwa kuoa wanawake wa kiarabu na wa makabila ya rangirangi, alikuwa na lengo maalum.
Shabaha ni kuondoa matabaka ndani ya jamii ya Wazanzibari. Jambo ambalo tunaweza kusema alifanikiwa.
Mchanganyiko wa ndugu wa damu wa makabili ya Zanzibar, unaooneka sasa ni wito na hekima za Mzee Karume.
Mzee Karume, tangu alipotoa wito huo miaka ya mwanzo baada ya mapinduzi mwiitikio ulianza wanaume kuoa wanawake wa kiarabu na makabila yaliyokuwa yakijiona ya rangirangi.
Mzee Karume (yeye menyewe) alianza kufungua milango ya kuoa wanawake wa kiarabu na wa rangirangi Pemba na Unguja. Pemba alioa wanawake wawili na Unguja alioa wawili.
Kadhalika, Mzee Jumbe baada ya kuwa Rais wa Zanzibar, alioa wanawake watatu wa kiarabu. Pemba wawili na mmoja Unguja. Alikuwa na wake wanne kwa wakati mmoja.
Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi (MBM) walianza kuoa Unguja na Pemba, kama alivyoagiza Mzee Karume.
Ali Muhsin wa ASP na Khamis Darweshi walioa wanawake ndugu, watoto wa Rashid bin Ali, Konde Pemba. 'Royal Family' ya Pemba.
Wafalme wa Zanzibar, kuanzia Sayyid Khalifa, Sayyad Abdullah na Sayyid Jamshid kila wakifanya ziara Pemba, walifikia kwa Rashid bin Ali wa Konde, ndiyo maana iliitwa 'Royol Family ya Pemba.'
Ali Muhsin alioa dada mtu (Raiyani) na Khamis Darweshi, alioa mdogo (Rauhiya). Wote walipata watoto. Hivyo, Ali Muhsin na Khamis Darweshi, watoto wao ni ndugu.
MBM mwingine aliyeoa mwanamke wa kiarabu Konde, Pemba ni Ramadhani Haji Faki. Naye alipata watoto. Pia kuna muungiliano wa damu.
Narudia; Tunaweza tukasema, watoto wa Ramadhan Haji, Khamis Darweshi na Ali Muhsin wa ASP wote ni ndugu. Hiyo ndiyo ilikuwa shabaha ya Mzee Karume.
Mkuatano mmoja wa hadhara wa Mzee Karume, uliofanyika 'Victoria Garden' mwaka 1966 na mikutano yake mingine alikuwa akisisitiza kwa wananchi wa Zanzibar, kuchanganya damu kwa kuoana ili kuondoa matabaka.
Shabaha ya Mzee Karume kutilia mkazo suala la kuchanganya damu alikuwa na dhamira ya kuondoa ubaguzi wa rangi na kabila na kuwafanya wananchi wa Wazanzibari kuwa ndugu wa damu, kuwa wamoja, bila kubaguana.
Kwenye mikutano yake ya hadhara alikuwa akisisitiza na kurudia mara kwa mara suala la watu kuchanganya damu kwa kuoa wanawake wa makabila ambayo kabla ya mapinduzi haikuwezekana.
Mbali na Mzee Karume na Mzee Jumbe viongozi wengine waliooa wanawake wa kiarabu na wa makabila ya rangirangi ni Ibrahim Amani, Rashid Abdalla Mamba, Hassan Nassor Moyo na Hamid Ameir.
Viongozi wengine ni Aboud Talib ambaye alioa mwanamke wa Kibulushi Wete, Ali Mzee Ali alioa mwanamke wa Mchangamdogo, Ibrahim Makungu alizaa watoto watatu na wanawake wawili tofauti wa Wete, Pemba.
Awali, ilikuwa ni aibu na fedheha wanawake wa kiarabu kuolewa na wanamapinduzi na viongozi wa ASP, ambao wengi welionekana kama hawafanani kwa mambo mengi.
Hata hivyo, kadiri siku zilivyosonga mbele, hali hiyo ilizoeleka, haikuwa tena jambo la ajabu na aibu kwa wazee wa wanawake hao. Kila kabila liliguswa na ndoa hizo.
Dk Ali Mohamed Shein na Seif Ali Iddi, miaka kumi waliyokaa kwenye madaraka hawakuliona hilo. Walishindwa kukumbuka shabaha ya Mzee Karume ya kuondoa aina zote za ubaguzi.
Uongozi wao, ulisimamia katika kuimarisha ubaguzi hadi kusahau dhamira na shabaha ya mapinduzi katika kuimarisha umoja wa Wazanzibari.
Marais wa Zanzibar wa awamu ya kwanza na ya pili na baadhi ya mawaziri wamewaunganisha wananchi wa Unguja na Pemba kwa damu tangu mwaka 1965.
Anapotokea kiongozi mbaguzi aina ya Dk Ali Mohamed Shein na swahiba yake Balozi Seif Ali Iddi ni hatari sana kwa nchi kama Zanzibar, ambayo watu wake takriban wote ni ndugu wa damu.
Lakini, wapo baadhi ya wanamapinduzi, hawakuoa wanawake wa kiarabu au wa makabila ya rangirangi. Mfano, Seif Bakari, Edington Kisasi na wingine.
Jambo jingine; Utamaduni ambao Unguja ulipuuzwa lakini, kwa upande wa Pemba uliendelea kuwepo, ni majina ya mitaa, njia, hospitali na skuli. Pemba, utamaduni huo umebaki mpaka leo.
Mfano, njia zote za Pemba, zimebaki na majina yake yale yale. Hospitali zote za Pemba, zimebaki na majina yake yale yale.
Isipokuwa Mkoani, 'Abdalla Mzee Hospital' ambalo ni jina la mtu aliishi ilipo hospitali yenyewe. Imejengwa baada ya mapinduzi.
Viwanja vya michezo, vimebaki na majina yake yale yale hata kiwanja kipya cha Gombani, kinaitwa kwa jina la mtaa kilipojengwa. 'Gombani Stadium.'
Mpika Tango cha Mkoani, Tibirinzi cha Chake Chake na Gombani ya Kale na vingine. Unguja kuna Mao Tse-tung. Chini kuna uwanja unaitwa Karume au Shamte? Upumbavu mtupu!
Mpaka mwaka 1972 njia kubwa za Pemba zilikuwa zimeekewa vibao: Ukiwa Mkoani (Chake Chake Road) ukiwa Chake Chake kuelekea Mkoani (Mkoani Road).
Ukiwa Mtambile kwenda Kengeja (Kengeja Road) Ukiwa Kengeja kwenda Mtambile (Mtambile Road) Ukiwa Chake Chake kwenda Wete (Wete Road) Ukiwa Wete kwenda Chake Chake (Chake Chake Road).
Ukiwa Wete kwenda Konde (Konde Road) Ukiwa Konde kwenda Wete (Wete Road) Ukiwa Wete kwenda Gando (Gando Road) Ukiwa Gando kwenda Wete (Wete Road).
Njia, mitaani na majego ya Pemba, vimebaki na majina yake ya awali. Isipokuwa kumbi za mikutano zilibadilishwa majina na kuitwa Jamhuri (Jamhuri Hall), na baadhi ya timu za mpira wa miguu.
Chake Chake kuna (Shamte Road) imetoka Miembeni imekatisha Bandataka na Kichungwani hadi Mahakama ya Chake Chake.
Njia hii ilifunguliwa na Sk Mohamed Shamte Septemba 1, 1963 miezi mitatu kabla ya uhuru wa Zanzibar wa Desemba 10, 1963.
Pia, kuna njia ya msingini (Msingini Road), ilikuwepo zamani na mwaka 1963 ilifanyiwa matengenezo makubwa.
Baadae ilifunguliwa upya na Mastari, kiongozi wa ASP na kuitwa (Mastari Road). Watu walishazoea 'Msigini Road.' Ilibaki kuitwa msingini hadi leo.
Soko kuu la samaki na nyama la Tibirinzi, Chake Chake lilifunguliwa rasmi March 16, 1963 na Sayyid Sir Abdullah bin Khalifa Al Said.
Kabla ya hapo samaki, nyama, matunda na mazao kama muhogo, viazi, ndizi na mazao mengine viliuzwa katika soko kuu la Chake Chake.
Soko jipya la samaki na nyama lilipewa jina la Mfalme huyo wa Zanzibar, na kuitwa (Sayyid Abdullah Market). Kwenye ukuta wa soko hilo yapo maandishi hayo mpaka leo.
Skuli ya Sekondari Vitongoji, Pemba ambayo baada ya mapinduzi iliitwa Fidel Castro ilifunguliwa na Sayyid Sir Jamshid.
Ilikuwa ifunguliwa na Sayyid Abdullah (baba yake Sayyid Jamshid), lakini alishapata ugonjwa wa mguu, aliwakilishwa na Sayyid Jamshid na kuitwa "Sayyid Abdaullah Secondary School".'
Skuli zote za Pemba, zilibaki na majina yake kwa maeneo zilipo;
Utaani, Mitiulaya, Jadida, Konde, Ziwani, Ole, Madungu, Michakaeni, Chanjamjawiri, Mtambile, Uweleni, Ng'ombeni, Kangani, Kengeja, Kiwani, Chambani, Shumba, Pandani na nyingine.
Ingawa kabla ya mapinduzi zipo baadhi nyingine zilikuwa za wasichana peke yao na nyingine wavulana peke yao. Mfano; 'Ng'ombeni Girls na Uweleni Boys' Chake Chake na Wete, hivyo hivyo.
Baadhi ya Skuli za Unguja, zilibadilishwa majina. Njia zilibadilishwa majini, Hospitali zilibadilishwa majina na kuitwa kwa majina ya nchi za nje au viongozi wa nchi za nje.
Pemba imefuata utamaduni wa Uingereza miji, mitaa, njia na skuli na taasisi nyingine zimabaki kama ilivyo asili yake.
Kwa mfano, akiulizwa mtu aliyezaliwa baada ya mapinduzi ya Januari 12, 1964 skuli gani mjini Unguja, ikiitwa 'Sayyida Matuka Secondary School?' Kwa asilimia 75 (75%) naamini hawataijuwa.
Wakiulizwa hao waliondoa jina la Bi Matuka na kuweka walilotaka wao wamepata faida gani? Hakuna faida yoyote isipokuwa ujinga mwingi!
Miaka ya karibuni baadhi ya wizara na taasisi za serikali zimekuwa zikifuata majina kwa mujibuwa wizara za serikali na taasisi za Tanganyika. Hivyo, Tanganyika wanaiga nini kutoka Zanzibar?.
Pemba, miji yake yote ilikuwa na huduma ya vyoo vya serikali (public toilets). Kabla na miaka michache baada ya mapinduzi, huduma hiyo ilitoweka.
Serikali imeufyata, kama si muhimu kuwepo wakati wananchi wanalipa kodi kupatiwa huduma hizo.
Kadhalika, mji wa Unguja, ulikuwa na huduma ya vyoo na huduma za kufulia nguo katika maeneo mengi, sasa labda kimebaki choo kimoja cha 'Darajani Taxi Stand.' Kama kipo, sina hakika.