KWELI Tangawizi inaweza kutumika kupunguza maumivu ya hedhi ya msingi (Primary dysmenorrhoea)

KWELI Tangawizi inaweza kutumika kupunguza maumivu ya hedhi ya msingi (Primary dysmenorrhoea)

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Wakuu

Je madai ya unywaji wa tangawizi kusaidia maumivu ya hedhi ni kweli? na je, kuna watu wamewahi ku experince hili?
1765347378101.png
 
Tunachokijua
Maumivu wakati wa hedhi kitaalamu hujulikana kama Dysmenorrhea (Menstrual Cramps), kwa mujibu wa Andiko lilochapishwa katika tovuti ya Cleverland Clinic ya nchini Marekani, ni maumivu ambayo mwanamke huyapata kipindi cha hedhi na huanza siku chache kabla ya hedhi na kupungua siku chache baada ya hedhi kulingana na mtu husika.

Maumivu wakati wa hedhi (Dysmenorrhea) yamegawanyika katika aina mbili ambapo aina ya kwanza ni maumivu ya hedhi ya kawaida haya ni maumivu yasiyo na sababu maalum katika kipindi cha hedhi, na aina ya pili ni maumivu ya hedhi yanayotokana na hali kama vile endometriosis ambapo Kwa mujibu wa tovuti ya medicover hospitals ni hali ambayo tishu zinazofanana na endometriamu hukua nje ya uterasi, mara nyingi kwenye ovari, mirija ya uzazi, au sehemu ya nje ya uterasi. Tishu hii huongezeka, kuchanika, na hutoka damu kwa kila mzunguko wa hedhi.

Tangawizi ni nini na faida zake kiafya?

Kituo cha Kitaifa cha Tiba Mbadala na Tiba Shirikishi cha nchini marekani (NCCIH) kupitia makala yake kinaelezea tangawizi, asili yake ni katika maeneo ya joto ya Asia, na sasa inalimiwa katika baadhi ya maeneo ya Amerika Kusini, Afrika na Mashariki ya Kati. Kihunzi chake (shina la chini ya ardhi) hutumika kwenye chakula na kwa madhumuni ya kiafya.

Tangawizi imekuwa ikitumika katika tiba za asili tangu nyakati za kale. Kienyeji, ilitumika kutibu hali mbalimbali kama pumu, mafua, mmeng’enyo wa chakula usio sawa, na usumbufu wa tumbo.

Kwa sasa, tangawizi inapendekezwa kwa ajili ya kichefuchefu na kutapika, osteoarthritis (maumivu ya viungo), maumivu ya hedhi, na hali nyingine mbalimbali.

Uhusiano wa matumizi ya Tangawizi na kupunguza maumivu ya hedhi

JamiiCheck imepitia tafiti na makala zinazoelezea faida ya matumizi ya tangawizi kiafya ikiwemo maumivu ya hedhi na kujiridhisha kuwa madai hayo ni ya kweli.

Ingawa tangawizi hiyo itakuwa na msaada kwa maumivu ya hedhi ya msingi ambayo ni maumivu ya kawaida na.

Utafiti uliofanywa na Pakniat na wenzake (2019) uliochapishwa na jarida la kitaaluma la Medicinal plants wenye kichwa "The Effect of Ginger on Primary Dysmenorrhea in Students of Qazvin University of Medical Sciences" ulihitimishwa kwa kueleza kuwa;

Matokeo ya utafiti yalionyesha kwamba dawa za asili kama tangawizi zina athari kubwa katika kupunguza ukali wa maumivu ya hedhi (dysmenorrhea).
Ingawa walipendekeza kufanyika tafiti zaidi ili kubaini kiwango sahihi cha dozi ya tangaweiz kwa ajili ya tiba kamili ya maumuvi ya hedhi n dalili nyingine za hedhi.

Utafiti uliofanywa na Ashmita Gurung na wenzake na kuchapishwa na jarida la kitaaluma la Clinical Epidemiology and Global Health wenye kichwa "Effectiveness of Zingiber Officinale (ginger) compared with non-steroidal anti-inflamamatory drugs and complementary therapy in primary dysmenorrhoea: A systematic review" Walihitimisha kwa kueleza
Matumizi ya tangawizi hadi gramu mbili kwa siku ni salama, ikigawanywa katika dozi ndogo ndogo za unga au kama sehemu ya chakula kwa muda wa siku tatu kuanzia siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi, inaweza kutuliza maumivu ya hedhi ya msingi
Ginger as ginger itself, or even tea made with ginger?
 
Pia ni chai na tiba Moja nzuri sana mjaarbu😜
 
Back
Top Bottom