heshima mbele wakuu.mimi napenda sana kuona watu wakikutana pamoja kwenye nchi za watu kama hizi party zinavyofanywa na huwa ni nyingi mno.sasa kwa vile ni nchi za nje na wengi wenu mnajiweza kidogo mara nyingi nimeona party nyingi zinaishia kukutana na kula ,,kucheza, kunywa na kujuana tumemaliza.
- Si kweli kwa sababu kuna ma-single kukutana kufahamiana mpaka kuishia kwenye ndoa, mifano ipo, kuna kusaidiana shule huenda shule yangu sio nzuri au malipo ni makubwa kuliko ya mwananchi mwenzangu hapa ninapata nafasi ya kubadilisha shule, mifano ipo, huenda kazi ninayofanya hailipi kama ya mwananchi mwenzangu ninahama kazi na kwenda kwenye malipo zaidi na mifano ipo, huenda sisi ni ndugu tumepoteana siku nyingi tunakutana na kuendeleza undugu na mifano ipo, huenda ninapoishi kuna wa-Tanzania wenzangu lakini sijui kama wapo tunakuatana kwenye hizi party na kufahamiana na majirani na mifano ipo, watoto wadogo kukutana na kufahamiana na mifano ipo.
- Halafu kumbuka kwamba huwa pia tunakutana wakati wa shida, sio sherehe tu kwa hiyo again mkuu bado unajaribu kulazimisha hoja, lakini uko out of the line na the spirit ya hizi sherehe.
mimi ushauri wangu mdogo tu,kwanini mnapokutana kwenye hizi party msipitishe kimchango flani yani sio lazima kwa wale walikuwa nacho chochote wachangie na huo mchango mue mnasaidia labda kwenye mahospitali nyumbani,au mashule ambayo hayana madawati na kadhalika.nadhani kama mkijaribu kufanya hivi mtakuta kwamba hizi party zina umuhimu mkubwa kuliko watu wanavyofikiria kwani mtakuwa wakati huo huo mnasaidia jamii nyumbani.ni wazo tu wakuu na nawatakia party njema.
- Mkuu wananchi wanapotaka kuchanga kusaidia jamii popote pale, inatakiwa iandaliwe kama Fund Raiser, lakini huwezi wananchi wanajaribu kustarehe kwa kutumia michango yao, ukaanza kupitisha bakuli eti kwa ajili ya shule za bongo, mkuu hapo kwenye party kuna watu kutoka sehemu ngapi za bongo?
- Je tutaanza kusaidia shule ya mwananchi gani na tutaacha ya mwananchi yupi? Kama wewe una shida ya kusaidia shule kwa njia ya party, basi tangaza party ya Fund Raiser useme na shule unayotaka kuisaidia, wananchi waje kwenye hiyo party wakijua wazi kwamba wanakuja kuchangia shule,
- Rais Mkapa, alipokuja kutuaga wananchi wa NYC kabla ya kuvua madaraka ya urais, alikuja na Rais wa sasa ambaye wakati huo alikuwa waziri wa nje na Rais mtarajiwa, katika ule mkutano pale Hermsely Hotel, akatokea bwana mmoja akamuuuliza Rais Mkapa, swali kama hili lako kwamba serikali ianzishe tabia ya kupokea michango toka kwa wananchi wa nje ili kusaidia kujenga bara bara ba kuweka umeme, lahaula la kwata Rais Kikwete akaomba kulijibu lile swali, nafikiri waliokuwepo wote wanakumbuka jinsi alivyotaka kushusha mbingu na majibu yake,
- Kwa kufupi tu alisema hivi, kama kweli mnazo hizo hela basi pelekeni msaidie vijijini kwenu na familia zenu kwa sababu serikali haihitaji hiyo michango ambayo haiwezi kumudu gharama za hata mti mmoja wa umeme, sasa mkuu mimi nikupe dola zangu mbili zikajengee shule kwenu, vipi kwetu? Kila kitu na wakati wake, kuna wakati wa kupanda na kuvuna, kuna wakati wa mvua na kiangazi, na pia kuna wakati wa sherehe na wakati wa Fund Raising, hatuwezi kuchanganya mambo,
- Point yako ni valid, lakini kama vile huko mwanzoni iko kwenye the wrong place, hapa sio mahali pake, anzisha mfuko maalum wa kusaidia shule Tanzania, na uweke ratiba za kuchangia uweke shule zote za Tanzania ambazo zitawakilisha wachangiaji wote, ninaomba uziache sherehe au party ziwe kama zilivyo yaani party za kusherehekea maisha ya wananchi kwa jasho lao. Hizi sherehe ni utamaduni ambao umekuwepo kwa miaka mingi sana, kila inapofika wakati wa Summer na mwisho wa mwaka na pia upo utamaduni wa kuchangiana wakati wa shida, au kusaidia jamii ndio maana meli ya MV. Bukoba ilipozama, tulikutana na kuchangia wananchi waliopona na tumewahi kufanya Fund Raising nyingi sana huko nyuma za namna hii na pia harusi za wananchi wenzetu, hizi tunafanya kila wakati sijasikia ukilalamika kama unavyolalamikia hii party, vipi kuna tatizo unashindwa kulisema wazi nini? maana haiwezekani ukawa hutaki tu kukubali mkuu sema tatizo lako badala ya kuendelea kuzunguka mbuyu, wote hapa ni watu wazima na tunajua namna ya kuchambua ishus betweeen the lines,
- Unaonekana una tatizo bigger than hii party kwa nini usiliseme tu mkuu, ukapatiwa majibu? Ila tu so far so good matayarisho yamepamba moto na wallahi hii party itakuwa ni kwa mtindo wa mdundo kama ule ambao ungetumika kwenye safari ya Tour ya mwisho ya MJ, yaani "This is it", kwa hiyo just see yah there!
Ahsante.
William.