Tangazo Hili la Vodacom linatia Aibu.

Tangazo Hili la Vodacom linatia Aibu.

iPad ya Apple

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
322
Reaction score
126
Ni Lille ambalo Mhindi anasikika aki pretend kumuagiza Juma ambaye ni mfanyakazi wake (Dreva)
akawachukue watoto wake Shuleni kumbe yeye anamaanisha mademu. Juma anamwambia mhindi naenda kuwachukua zen yule mhindi anamwambia Kuwa waambie watoto natuma pesa kwa M Pesa, Dreva anababaika lakini mhind anaishia ku mwambia Jumaaaa totoooo,totoooo Juma hijui totooo? Juma chumbani totoooo!!! Baada ya hapo Juma anagundua Kuwa Bosi anamaanisha wasichana. Kwa kweli hili Tangazo linabore sana pale linaposikika ukiwa umekaa na mzazi wako hasa wa jinsia ya tofauti na yako.

My take, Ni bora Vodacom wakaangalia namna ya Kuwa na matangazo mazuri, kuliko hili linaloleta fedheha katika sebule za watu. waige ubunifu wa Airtel ktk matangazo Kama lile la Hamia Airtel, Airtel ya tosha na hihi ya Hakatwi mtu hapa.
 
Wabongo matangazo yanayoashiria ngono ndo huwa mnayapenda sana hadi mnayaanzishia thread....
 
Ipad,

I support you. Nadhani kuna maadili ambayo hawa wafanyabiashara wanatakiwa kuyazingatia wanapoandaa matangazo, na pia nadhani ni muhimu kuzingatia uhusiano wa mambo/elements katika tangazo lenyewe. Kwa hapo nadhani inaweza kutafsiriwa kuwa Vodacom wanakubaliana na suala la watu wazima (sugar dadies) kuwatongoza watoto walio shuleni. (jambo ambalo siyo lengo la Voda). Aliyeandaa tangazo alilenga zaidi kuwavutia/kuwaburudisha wasikilizaji hadi akasahau kuzingatia maadili/maudhui. Mtazamo wangu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
JF weka katangazo kenye picha ya skirt ama tangazo la hovyo kwenye MMU uone litakavyosomwa na wengi,Logwa uweke kwenye Siasa utawapata wale vichwa ngumu tu,kwa hiyo wameshafanya utafiti na wamegundua hadhira inataka kusikia nini...Beside maadili yameshaporomoka miaka 38 iliyopita...
 
hili tangzo inabidi liwe linarushwa usiku wa manane ili watoto wetu wasijifunze mambo ya wakubwa.
 
Ipad,

I support you. Nadhani kuna maadili ambayo hawa wafanyabiashara wanatakiwa kuyazingatia wanapoandaa matangazo, na pia nadhani ni muhimu kuzingatia uhusiano wa mambo/elements katika tangazo lenyewe. Kwa hapo nadhani inaweza kutafsiriwa kuwa Vodacom wanakubaliana na suala la watu wazima (sugar dadies) kuwatongoza watoto walio shuleni. (jambo ambalo siyo lengo la Voda). Aliyeandaa tangazo alilenga zaidi kuwavutia/kuwaburudisha wasikilizaji hadi akasahau kuzingatia maadili/maudhui. Mtazamo wangu.

Mungu ibariki Tanzania.

Upo sahihi Kabisa mkuu.
 
na lile tangazo la airtel la baba lao. linaboa sana yan. inabid wajipange sana.
 
Ushindani wa kibiashara umekuwa mkubwa sana haswa kwenye kampuni za simu hadi wanasahau maadili. Tatizo wanajali kupata faida kwa hiyo wako tayari kufanya lolote ambalo wanadhani litawaingizia faida. Kwangu mimi wahusika wamepoteza mwelekeo kwani wameshindwa kuwatambuwa wateja wao ni akina nani na mahitaji yao ni yepi period. Wajipange upya.
 
Kiukweli mara ya kwanza nilipolisikia nilijiuliza sana wamekubaliwa vipi kurusha tangazo linalochochea UZINZI!!!!
 
Mbona matangazo ya ndumu hamyasemi kuwa yanachochea uzinzi??? au yale yako poa?
 
Si hilo tu kuanzia hizi local radio tv karibu zote kuna matangazo ya kipuuzi sana ambayo yaanathari kubwa kwa watoto wanaokuwa,jaribu kufatilia matangazo ya pombe matangazo ya condom uone yalivyo ya kipuuzi kabisa,hizi radio local zimekuwa zinaongoza kwa kushangilia upuuzi kabisa,tumekuwa jamii isiyo na mtazamo,tunashindwa kufaham mtoto alie chini ya umri wa miaka15 akili yake si sawa na mtu mzima,yeye anapokea chochote kama kinavyokuja bila kuchuja,lawama inatakiwa ianzie ndani ya family na jamii yote bila kusahau serikali iliyo usingizini
 
Mbona matangazo ya ndumu hamyasemi kuwa yanachochea uzinzi??? au yale yako poa?

Mkuu, 'ndumu' ni nini? Kuna jambo inabidi kwenye taifa letu tukubali kubadilika. Kwa mfano kwenye hiyo comment yako, watu ulioona wanachangia hapa wanazungumzia kuhusu mada iliyoletwa na huyu ndugu hapa (kuhusu hilo tangazo la Voda), hawajazungumzia hizo "ndumu" kwasababu mjadala ulioanzishwa hapa ni specific. Sasa, wewe usianze kuuliza mbona hili hamsemi mbona hili hamsemi, ni vyema wewe ukatoa mtazamo wako kuhusu mada uliyoikuta hapa, na kama unataka kuuliza kuhusu hizo "ndumu" basi unaweza kuanzisha mada mpya (unaruhusiwa). Usiwe "negative" sana mkuu.Usiwe wa kutafuta kukosoa tuu kila unapoona jitihada za watu hata katika maeneo mengine ya maisha yetu. Be positive tuweke mchango kwenye maendeleo yetu.

Amani kwako.
 
...Bado Linaendelea. Inaonekana miongoni mwa Wahusika hakuna Member wa JF. Sad.:disapointed:
 
Mtu kimtokacho ndicho kimjazacho hawa Voda inaonekana wamejawa na fikra za ngono ndiyo maaana wanadiriki kupeleke tangazo hewani lenye upuuzi kama huu,upande wa pili wako wapi TCRA kukemea na kuadhibu tabia kama hizi au wapo kuchukua ushuru wa leseni tu ? tusipokuwa makini maadili hata kidogo yaliyopo yataisha.
 
--*kinachotakiwa ni UJUMBE wa M-Pesa umefika kwa walengwa?
iwe Dreva, Driver, dereva hata totooooo
je walengwa wamevutika?
yote tisa
Airtel Money hii ndio huduma murua maana hakatwi mtu yeyote
na sijui faida na Kodi wanapataje
lakini watu wanaikandia kwa kusema hakatwi suna jando mtu hapa na wengi wakiwa na lengo la kuwaponda Airtel
Kwa hiyo haya Makampuni ya simu yapo kimashindano waacheni wajitangaze na km ujumbe mmeugundua una matusi waapima wao unavyoathiri biashara yao au Wananchi

Back
Top Bottom