Tangazo Hili Lina Mapungufu Ya Lugha!

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Kuna tangazo linarudiwarudiwa sana kwenye kituo cha televisheni ya star (startv).Tangazo linahusu ubora wa king'amuzi cha continental.
Anayekisifia king'amuzi hiki anatoa maneno mengi ya sifa huku akisema:"King'amuzi cha continental kiko vizuri sana, tena hakisklachisklachi, ni klia kabisa"

Imekuwaje wahusika wa tangazo hili wakaridhika na lugha iliyotumika kwenye hayo maneno niliyobold? Lipo neno la kiswahili sanifu linaloweza kutumika kuelezea dhana iliyomo kwenye neno nililobold.

Sklachi ni matamshi mabovu ya neno la kiingereza 'scratch'. Kiswahili fasaha ni 'kukwaruza'

Huyo mtangazaji (ni mhusika pia kwenye komedi ya futuhi) alitakiwa aseme: "hicho king'amuzi hakikwaruzikwaruzi.
Angesema hivyo ningejisikia vizuri sana.
 
Kuna radio station Arusha inaitwa Sunrise........ukisikiliza unaweza tapika........kuna dada mmoja na mkaka wao matumizi ya L na R hayawahusu.........nyie mnaosikiliza mtajijua.........
 
Wakati mwingine hizo lugha zinaookosewa kwa makusudi ndio ubunifu na uzuri WA tangazo. Shangaa kwa nini pia herufi za coca cola huwa zimeungana na kunyongwa kwenye ile logo. Yao. Kwa nini wasingeziachanisha mojamoja.Wamekosea au?
 
Ndugu hiyo ya mchoro wa cocacola imefanyika intentionally as a graphic design.Je wataka niambia kusklachisklachi nayo imetamkwa intentionally kupamba matamshi?
 
Kuna radio station Arusha inaitwa Sunrise........ukisikiliza unaweza tapika........kuna dada mmoja na mkaka wao matumizi ya L na R hayawahusu.........nyie mnaosikiliza mtajijua.........
Namshukuru Mungu siishi Arusha kwa hiyo hicho kituo sijapata kukisikiliza! Matamshi yanayochanganya 'l' na 'r' yananileteaga aina ya ka-ugonjwa fulani hivi - najisikiaga vibaya sana mtu anaposema kwa mfano:Mgonjwa wa marelia amebebwa na roli kwenda hospitali!
 
Yananileteaga.?????=yananiletea ndio neno sahihi..!
 
Mkuu hiyo ni sanaa tu...inaonekana mtu anayeongea ni mtanzania wa kawaida maana kwa hakika ndivyo tunavyoongea. Wangetumia kiswahili sanifu tangazo hata lisingevutia
 
mkuu kama hujiskii vizuri nenda kapime mkuu, labda una malaria..
 
Ndugu hiyo ya mchoro wa cocacola imefanyika intentionally as a graphic design.Je wataka niambia kusklachisklachi nayo imetamkwa intentionally kupamba matamshi?
Ndugu,hata kwenye matangazo ya sauti kuna usanii wake WA kuumba maneno ili kumvutia msikilizaji. Umelisikia tangazo moja la tigo linalosema 'jismartishe na tigo' kwani hawakupata neno la swahili sanifu hapo? Ukitumia kiswahili sanifu muda wote na hasa kwenye matangazo hautaona ladha ya kusikiliza!
 
Kwenye hilo tangazo la Tigo wamenyambua neno smartphone kuwa jismatfonishe.Upo ubunifu wa kuvutia hapa lakini si kwenye kusklachisklachi
 
Hata wewe umekosea,Sahara media hawana king'amuzi cha continental bali wana kisimbusi cha continental.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…