Tangazo kutoka chuo cha uhasibu arusha

Tangazo kutoka chuo cha uhasibu arusha

JAFE

Senior Member
Joined
Sep 1, 2012
Posts
191
Reaction score
42
550017_434363423316633_1373669124_n.jpg

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

Kutokana na Chuo kufungwa, Baraza la Uongozi wa Chuo
katika kikao chake cha dharura cha tarehe 03 Mei 2013
kimeagiza wanafunzi wote kuanzia ngazi ya Cheti mpaka
Stashahada ya Uzamili kuzingatia yafuatayo:

1. Kila Mwanafunzi anatakiwa kutuma maombi mapya ya
kujiunga na Chuo.
2. Barua ya maombi hayo ipitishwe kwa Mkuu wa Wilaya
anapoishi mwanafunzi. Kwa mwanafunzi wa Stashahada
ya Uzamili ya Uhasibu barua yake ya maombi ipitie kwa
Mhasibu Mkuu wa Serikali.
3. Katika maombi hayo mwanafunzi anaagizwa kueleza
namna alivyoshiriki katika vurugu za tarehe 24 Aprili
2013.
4. Mwanafunzi awe amekamilisha malipo ya ada iliyobaki
wakati anatuma maombi yake.
5. Mwisho wa maombi ni tarehe 16 Mei 2013.
Maombi yapelekwe kwa anwani ifuatayo:
Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Uhasibu Arusha
S. L. P. 2798
Arusha.
08 Mei 2013
TEMBELEA TOVUTI YA CHUO
www.iaa.ac.tz
kwa taarifa zaidi
endelea kupitia
http://audifacejackson.blogspot.com




 
Mbona haya masikhara jamani? sasa kuna fujo ama vurugu zilizofanyika pale kweli?hivi hawa viongozi wa vyuo wana watoto kweli? hivi wanamjua Mungu? hivi wangekuwa watoto wao wangefurahia? hivi ni lini haya yatakoma tanzania? hivi ni lini viongozi wataacha unafiki kwenye maamuzi kama haya? mbona haya yanatokea Tanzania?
 
...Ama kweli akili ndogo zinapotawala akili kubwa ni shida kwelikweli. Naona 2015 inakuwa mbali sana!
 
Hii ndio nchi inayojitamba kwa siasa yenye miiko ya kidemokrasia
 
Huo ni kupiga "Msasa" au wanafundisha vijana kuwa na Discipline ?
hali ngumu !!
 
Mchawi akishindwaga kuroka huanza kuropoka ropoka ovyo ndio mfano wa haya. Yetu macho.
 
eti wanafunzi walileta fujo......Tanzania kuna vituko sana
 
Kwa hiyo ndo tuseme tunatuma maombi ya kujiunga na chuo kama vile hatukuwahi kuwepo chuoni. Cjaelewa.
 
Hivi hawa waliokaa na kuamua haya mambo walifanya maamuzi haya kwa mtutu wa bunduki au kwa akili zao? Maana waliyoyaamua hayana mashiko na yamejaa ukomoaji na siasa badala ya kuweka taaluma mbele, uongozi huu wa chuo umeamua kutumika kisiasa.
 
Dah!Hili tangazo kama limeandaliwa na watoto.
 
Ama kweli baadhi ya Vyuo Tanzania ni sawa ni vituo vya mitihani.......yaani hili nalo jambo la kupitia milolongo yote hiii!!!!!!!!! Hapa lazima Mulongo ana mkono wake.
 
Wala msiogope hata sisi pale UDSM mwaka 2007 tulifanyiwa hayohayo na tukaendelea kugoma tu.aluta continua.
 
mbona haya masikhara jamani?sasa kuna fujo ama vurugu zilizofanyika pale kweli?hivi hawa viongozi wa vyuo wana watoto kweli?hivi wanamjua Mungu?hivi wangekuwa watoto wao wangefurahia?hivi ni lini haya yatakoma tanzania?hivi ni lini viongozi wataacha unafiki kwenye maamuzi kama haya?mbona haya yanatokea tanzania?
Kuna tetesi kwamba wanataka kutengeza Hadithi nyingine kutokana na barua za maombi za watakaoomba kupitia kwa mkuu wa wilaya na Mhasibu mkuu wa Serikali, yaani watatangaza Bungeni kwamba wanafunzi wengi wamesema Lema ndiye aliyewatuma na wanajuta kwanini hajawasaidia kurudi chuoni.
 
Kuna tetesi kwamba wanataka kutengeza Hadithi nyingine kutokana na barua za maombi za watakaoomba kupitia kwa mkuu wa wilaya na Mhasibu mkuu wa Serikali, yaani watatangaza Bungeni kwamba wanafunzi wengi wamesema Lema ndiye aliyewatuma na wanajuta kwanini hajawasaidia kurudi chuoni


Hapo kwenye red hujakosea hata nukta

Ila kuzuia mabadiliko yanapotaka kuja ni ngumu sana.....zaidizaidi heshma yao inazidi kushuka
 
Back
Top Bottom