Tangazo kwa Umma juu ya uuzaji wa viwanja katika eneo la Golani, kata ya Kimbiji

mour

New Member
Joined
Mar 28, 2013
Posts
1
Reaction score
2
TANGAZO KWA UMMA JUU YA UUZAJI WA VIWANJA KATIKA
ENEO LA GOLANI KATA YA KIMBIJI NA YALE YALE PUNA
KATA YA PEMBA MNAZI

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Kampuni ya Ardhi Plan inatangaza kuuza viwanja 1500 vilivyopimwa katika eneo la Golani kata ya Kimbiji jirani na kambi ya JKT na Yale Yale Puna Kata ya Pemba Mnazi.
Viwanja vyenye ukubwa na matumizi mbalimbali vitauzwa kwa mujibu wa bei zilizopo katika jedwali la hapo chini kwa utaratibu ufuatao:-

I) Fomu za maombi ya kumiliki kiwanja hazitalipiwa.
II) Idadi ya fomu zilizoandaliwa inalingana na idadi ya viwanja vilivyopo.
III) Fomu za maombi ya kumiliki viwanja zitatolewa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 9 Alasiri tarehe 02.04.2013 katika ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
IV) Mwisho wa kurudisha fomu zilizojazwa kwa ukamilifu ni tarehe 08.04.2013 saa 9 Alasiri.
V) Ankara za malipo (Vocha) pamoja na mwongozo wa kulipia viwanja zitatolewa kwa mwombaji atakayerudisha fomu kwa muda uliopangwa.
VI) Malipo yalipwe kwa mkupuo ndani ya siku 21. Mwombaji ambaye hatakuwa amefanya malipo kwa muda uliopangwa kiwanja husika kitatolewa kwa mwombaji mwingine bila ya taarifa yoyote kwake.
VII) Viwanja vilivyopangwa kwa ajili ya makazi vina ukubwa kama ifuatavyo:

Na. Aina
1. Ujazo wa juu (High density)-Ukubwa (M²) 300-600 -Idadi 761
2. Ujazo wa kati (Medium density) -Ukubwa (M²) 601-1200 -Idadi 617
3. Ujazo wa chini (Low density) -Ukubwa (M²) 1201-2500 -Idadi 52

JEDWALI: VIWANGO VYA GHARAMA YA VIWANJA KWA MATUMIZI MBALIMBALI

1. Makazi pekee(Ujazo wa juu, kati na chini) 8,000/=
2. Makazi na biashara 8,000/=
3. Biashara (Hotel, Vituo vya mafuta, maduka makubwa) 10,000/=
4. Huduma za jamii (Zahanati, shule ya awali, sekondari) 8,000/=
5. Ibada/kuabudu 8,000/=
6. Makazi maalumu (Housing Estate) 8,000/=

NB KWA WALE WATAOWEZA KUNUNUA GAZETI LA MWANANCHI LA JUMANNE, MACHI 26,2013 UKURASA WA 8 (NANE) KUNA TANGAZO HILI PIA, PIA TANGAZO HILI UMAWEZA KULIPATA KWENYE WEBSITE: Home | Ardhi Plan Ltd
 
Asante sana mkuu
tatizo ni urasimu wa kupata viwanja hivyo.
Maana kuna watu wameshanza kuuza vocha za viwanja hata kabla ya zoezi la ugawaji kuanza.
 
Am not sure kama hizo bei sahihi!!!
 
Hii bei mbona ipo juu sana

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hongera JF kwa kazi nzuri, this time wamejifunza; Idadi ya form ni sawa na Idadi ya Viwanja vitakavyotolewa; Form ni bure hili lilijadiliwa sana hapa JF kipindi kile cha viwanja vya Gezaulole
 
Jamani kuna yeyote aliyefuatilua hivi viwanja? Mama yangu ameenda leo jumatano April 3rd na kuambiwa kuwa fomu zote zimeshaisha. Sijuini kweli au ndio utapeli tu... Mwenye info zaidi naombeni maelezo plz
 
marango naomba unieleweshe juu ya jambo hili maana naona bei zake ni ndogo na unasema zipo juu, naomba unieleweshe hizo bei zina present kitu gani au inabidi uizidishe?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
marango naomba unieleweshe juu ya jambo hili maana naona bei zake ni ndogo na unasema zipo juu, naomba unieleweshe hizo bei zina present kitu gani au inabidi uizidishe?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

hiyo ni bei kwa mita moja ya mraba.Kwa hiyo ukichukua chenye ukubwa wa 1200 maana yake unazidisha na hiyo bei ya ukubwa wa kiwanja ulichochagua.mf 1200*8000=9,600,000?=
 
Jamani kuna yeyote aliyefuatilua hivi viwanja? Mama yangu ameenda leo jumatano April 3rd na kuambiwa kuwa fomu zote zimeshaisha. Sijuini kweli au ndio utapeli tu... Mwenye info zaidi naombeni maelezo plz

Mkuu mimi nilienda pale tar 02/04 na watu walikuwa wengi sana zaidi ya idadi ya form. Wengine walilala pale wakisubiria form. Ni kweli form ziliisha siku ile ile mkuu
 
Ndo utekelezaji wa mradi mji mpya umeshaanza?
Hizi ndo double standard kwa kweli. Iko wapi Kigamboni Development Authority?
Wanunuzi jiangalieni msije kutapeliwa, maana kigamboni haipo chini ya manispaa ya temeke tena tangu January mwaka huu.
 
Subiria walanguzi wataanza kuziuza soon. Manake watapewa ofa na hawana hela za kulipia.
 
thanks king'asti, nadhani wauzaji lazima watafute mbinu nyingine, hawa walanguzi huwa wananunua vocha halafu wanaanza kulangua kama wanauza viwanja mwisho wa biashara unakuta viwanja nusu havina watu lakini pesa imeliwa na madalali feki

ndilo tatizo lililopo mwongozo kigamboni, hakuna kinachoendelea na hadi leo washenzy wanauza viwanja
 
Subiria walanguzi wataanza kuziuza soon. Manake watapewa ofa na hawana hela za kulipia.

Hivi viwanja sio vya serikali, mtu asipolipa ndani ya majuma matatu kiwanja kinauzwa fasta.
 
Hivi viwanja sio vya serikali, mtu asipolipa ndani ya majuma matatu kiwanja kinauzwa fasta.

good one

ila kaa ujue maafisa ardhi wanaongoza kwa sabotage ya mauzo hayo maan watawaambia watu viwanja vimeisha wakati mhusika hajauza
 
Jamani kuna yeyote aliyefuatilua hivi viwanja? Mama yangu ameenda leo jumatano April 3rd na kuambiwa kuwa fomu zote zimeshaisha. Sijuini kweli au ndio utapeli tu... Mwenye info zaidi naombeni maelezo plz
Baada ya Sisi wananchi kulalamika kua Serikali imekua ikitutapeli kwa kutoa fomu labda 30,000 wakati viwanja havifiki viko labda 600 tu, sasa wamejirekebisha kwa hili kwa kutoa form zinazolingana ma idadi ya viwanja ili kusiwepo na watakaonunua form kisha wakose viwanja.

Ndio kusema kua ukibahatika kupata form ndio umepata Kiwanja, labda uwe huna hela.

Ni aina nzuri ya uuzaji viwanja, labda tatizo lije kua kama wameamua kutumia style hii sasa, je sisi tuliokosa viwanja kwa style ile ya zamani turudishiwe hela zetu??
 
Ninachotaka kujua kwanini viwanja vya kigamboni bado vinauzwa kupitia manispaa ya Temeke na si Kigamboni Development Authority tuliyotangaziwa kupitia vyombo vya habari kwamba imeanza kazi tangu January 2013? Afu maeneo hayo uliyotaja si ndio yaliyoongezwa juzi kwanye mpango mkakati wa Kigamboni new city?

Mkuu kama kawaida yao,sasa hivi form zinalanguliwa kwa kwenda mbele,jamaa angu ameambiwa kama anataka inabidi amlipe alie na form bei mara mbili ya bei iliyowekwa na manispaa.
Jamani kuna yeyote aliyefuatilua hivi viwanja? Mama yangu ameenda leo jumatano April 3rd na kuambiwa kuwa fomu zote zimeshaisha. Sijuini kweli au ndio utapeli tu... Mwenye info zaidi naombeni maelezo plz
 
Nashukuru kaka kwa maelezo yako na kunipa ufahamu 🙂

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…