Tangazo la ajira la TAMISEMI lina mkanganyiko kwa watu wenye ulemavu

Tangazo la ajira la TAMISEMI lina mkanganyiko kwa watu wenye ulemavu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Maombi ya nafasi za kazi kada ya Afya na Elimu yameanza kupokelewa na TAMISEMI lakini kuna mkanganyiko ambao nimeuona kwa watu wenye ulemavu. Kwa namna ya kuomba.

1. Japo maombi yanapashwa kupitia kiunga cha ajira.tamisemi.go.tz maombi kwa watu wenye ulemavu yametakiwa kutumwa kwa 'nakala ngumu'(Hard copy) Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu

2. Agizo linalofuata ni kuwa maombi kwa njia ya posta na yatakayopelekwa kwa mkono hayatazingatiwa, hali ambayo inaweza kuleta shida zifuatazo.

Je, watu wenye ulemavu watume Ofisi ya Rais TAMISEMI mtandaoni tu?

Watume kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu tu (Kwa hard copy) njia ya posta.
Au watume kwa Katibu Mkuu kwa Hard copy na kutuma maombi Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Screenshot 2022-04-21 at 09-47-41 TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI 2022.pdf.png


Niwatakie kila la kheri wanaoomba nafasi za kazi zilizotangazwa, ni matumaini yangu TAMISEMI watakuja na ufafanuzi wa hili jambo
 
Afu Kuna dogo namfanyia application mbona kwenye Ku click fungua account inagoma?? Why??
 
hujaelewa nini? na miaka yote tangazo linaenda krbu hivyo hivyo tofauti ni ndogo ambazo hutoa fursa watu kuomba...
 
address ina jieleza ziende kwa mkurugenzi wa idara husika... wengine mkituma kwa posta hazito shughulikiwa sababu sio walemavu... na kumbuka ktk bahasha una andika aione mkurugenzi idara husika...
 
Hizi web apps za hapa nyumbani (made in Tanzania) nyingi si compatible kweenye mobile browsers

Tupia PC au kwenye mobile browser set "PC site" option
Mtu yuko Idindilumunyo, Igodivaha, Kiyavitende and the like atayajulia wapi hayo, kuna watu wako kwenye disadvantaged zones amba hali ya uchumi siyo rafiki na hata upatikanaji wa mtandao ni changamoto

Akiandika barua anaagiza kwenye bus ikatumbukizwe posta ndiyo angalau kwake

Screenshot_20220421-152046_Samsung Internet.jpg
 
Hizi web apps za hapa nyumbani (made in Tanzania) nyingi si compatible kweenye mobile browsers

Tupia PC au kwenye mobile browser set "PC site" option
Mkuu TAMISEMI walitakiwa kutazama vitu kama hivyo in advance maana ni technical si watu wote wanaojua vilitakiwa viandikwe kama mwongozo kwa waombaji, vinginevyo wengi watakatishwa tamaa wataishia njiani
 
Hizo ajira kipaumbele watapewa watu wa jimboni kwa Ummy Mwalimu. Ni kama tu Jaffo alivowapa kipaumbele vijana wa Kisarawe kwenye ajira za Ualimu
 
nina uemavu wa miguu, natarajia kujiunga na udom mwaka huu sijui maisha yakoje huko, yeyote mwenye experience ya kusoma na haii chuoni hapo au anayemfahamu aliyesoma /anayesoma hapo na hali km hio please naomba ani PM contacts zake, natanguiza shukrani
 
Back
Top Bottom