Tangazo La Maandalizi ya Ndoa

Jumanne Jioni sina uhakika sana but nipe mawasiliano yako ili niwe nayo kwanza ntakushtua ila kikao kingine ni Jumamosi hii tarehe 10 kuanzia saa 11 pale Kilimanjaro Park , Mbele ya Mwika Hall

Naomba baada ya kikao cha "harusi" mfanye mpango wa kufanya kikao cha kufanya usafi "makaburi" yaliyoko "opposite" na hizo baa ulizozitaja. Inashangaza watu wanavyofanya starehe za ajabu mbele ya makaburi bila kuwa hata na "wazo la pili".

Tubadilike - SAY NO: Kuchangia shughuli za anasa:
 
Harusi siyo ati kama bethdei pati..Kiafrika harusi ni shughuli ya familia,ndugu jamaa na marafiki kama msiba.Usijaribu kuonyesha hiyo jeuri hata kama una pesa... utajikuta unasusiwa mazishi ndugu.Utalia sana likikufika... si una pesa?

Tausi

Ulishawahi kuchangia lipi kati ya haya yafuatayo:-

- Matibabu ya rafiki yako mgonjwa?
- Elimu ya mtoto wa rafiki yako
- Ujenzi wa zahanati

Mimi siwezi kuchangia "shuguli" inayoisha baada ya "shughuli": Hii mnayoita "utamaduni wa kiafrika" kwangu mimi ni "utamaduni wa kijinga"!

Huwezi kumchangia mtu "kuoa" say Tshs 200,000: wakati mtu huyo huyo anaye mdogo wake ambaye anakosa Tshs 100,000 za ada ya shule au Mama yake mzazi kule kijijini hana Tshs 50,000 ya matumizi madogo madogo: that is imbecility of highest order!

Mimi nimeoa bila kufanya "vikao vya Harusi" na bila "kuchangiwa". Nilifunga ndoa 10years ago Kanisa la Mt Joseph Dar es Salaam asubuhi na baada ya hapo sherehe ilifanyika nyumbani kwangu: Waliofika ndugu jamaa na Marafiki wenye "mapenzi mema".

Kwa wale wanywaji: Kila mmoja alikuwa anaagiza kwa "pesa yake" kutoka Baa ya Jirani na Chakula kiliandaliwa na majirani.

Nipo na Mke wangu for 10 years now blessed with two kids - hutujawahi kwenda "kusuruhishwa" kwa Padri au Wazee wa kanisa - hata siku moja.

TUBADILIKE: Ndoa imara haijengwi kwa Michango ya Harusi - SAY NO to Michango:
 
Kama mwanajamii nimetimiza wajibu wangu kuwajulisha wanajamii wenzangu kuhusu malengo yangu hayo kwahiyo kuchanga au kuchangia au kuwa sehemu ya wanajamii wanaopenda kuwa kwenye kamati ya kufanikisha shuguli hii sio lazima -- lakini ni lazima mimi kutimiza wajibu wa kutaaribu jamii na nimeshafanya hivyo hivyo vingine ni juu ya mwanajamii mwenyewe kuamua
 

umeongea yote, hongera for your perfect marriage
 

Ok bwana harusi mtarajiwa tumekuelewa:violin:
 

Nafikiri haya ni maandalizi ya sherehe ya ndoa yako yaani harusi! Maandalizi ya ndoa yako walianza wazazi wako na wewe mwenyewe toka siku nyingi! Je, unaweza kutupa sababu za msingi za wewe kuoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…