tausi
ulishawahi kuchangia lipi kati ya haya yafuatayo:-
- matibabu ya rafiki yako mgonjwa?
- elimu ya mtoto wa rafiki yako
- ujenzi wa zahanati
mimi siwezi kuchangia "shuguli" inayoisha baada ya "shughuli": Hii mnayoita "utamaduni wa kiafrika" kwangu mimi ni "utamaduni wa kijinga"!
Huwezi kumchangia mtu "kuoa" say tshs 200,000: Wakati mtu huyo huyo anaye mdogo wake ambaye anakosa tshs 100,000 za ada ya shule au mama yake mzazi kule kijijini hana tshs 50,000 ya matumizi madogo madogo: That is imbecility of highest order!
Mimi nimeoa bila kufanya "vikao vya harusi" na bila "kuchangiwa". Nilifunga ndoa 10years ago kanisa la mt joseph dar es salaam asubuhi na baada ya hapo sherehe ilifanyika nyumbani kwangu: Waliofika ndugu jamaa na marafiki wenye "mapenzi mema".
Kwa wale wanywaji: Kila mmoja alikuwa anaagiza kwa "pesa yake" kutoka baa ya jirani na chakula kiliandaliwa na majirani.
Nipo na mke wangu for 10 years now blessed with two kids - hutujawahi kwenda "kusuruhishwa" kwa padri au wazee wa kanisa - hata siku moja.
Tubadilike: Ndoa imara haijengwi kwa michango ya harusi - say no to michango: