Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,523
- 30,084
Tangazo linalotolewa na chama cha waingizaji wa gesi ya kupikia(TZLPGA) haitatui matatizo yanayotupata watumiaji wa gesi ya kwenye mitungi ikiwemo ujazo na ubora wa vichomea(burner).
Vichomea vilivyopo mitaani ni vya viwango vyachini pamoja na uwepo wa TBS na Tume ya Ushindani, vingi yya vifaa hivi hujiongeza vyenyewe uvitumiapo na baadhi hufikia viwango hatari vinavyo weza kusababisha ajali ya moto.
Lipo tatizo lingine ambalo ni rahisi kulidhibiti lakini hakuna utashi, nalo linahusu ubora na ujazo wa gesi kwenye mitungi, utashi ni waingizaji kuwa na sharti la kuweka vichomea(burner) vyenye dira (mita) inaoonesha ujazo na upungufu unaotokana na matumizi licha ya watumiaji kulalamika kila siku bila kusikilizwa na mamlaka zinazosimamia kutokana na kukosa utashi.