Tangazo la Wizara ya Ardhi la Rais kutwaa ardhi Dar ni matokeo ya Mipango miji ya kisiasa. Nchi haileweki wala haina plan za miaka hata 20 ijayo

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Wakati wenzetu wakiwa na plan za miaka 100 ijayo Bongo tuna plan za wiki 5 zijazo. Nchi ina plani za kisiasa na ziko Surported na wajinga hili Taifa la Tanzania.

Tanzania kuna plan za wiki chache mbele, kila mara ni Bomoa hiki weka hiki, badili hiki weka hiki.

Mfano Chukulia ujenzi wa kituo cha Mabasi cha Ubungo wale wahuni walitarget miaka mingapi mbele? Angakia sasa kituo kisha kufa kimepewa majukumu mapya ambayo hayakuwepo kabisa.

Ile Mbezi kituo cha Mabasi baada ya miaka 7 kuanzia sasa itaonekana ni pafinyu sana,pako mjini sana katikati sana hivyo wanatafuta eneo jipya wahamishe stendi na pale wajenge hata soko la wamachinga, na sisi Wajinga tutashangilia sana mno.

Raisi anatwaaa aridhi Dar kisa ujenzi wa miundo mbinu ya mabasi yaendayo kasi, sasa jiulize Nchi nzima hakuna alie kuwa anawaza kitu kama hchi miaka 30 iliopita?

Tuombe uzima baada ya miaka kadhaa itaonekana tena hizo Barabara za mwendo kasi hazifai watavunja wajenga njia za treni za kuzunguka Dar na pia watatwaa aridhi.

Miji inajengwa kiholela sana, miji imejaaa frame, miji haina maeneeo ya akiba, miji imejaaa majengo tupu, miji ina plan za mwaka mmoja mmoja mbele.

Sijui nani alieawadanganya Watanganyika kwamba miji ni majengo yenye Frame, make miji imejaaa mno Frame hakuna space tena.

Fikiria jiji kama New york Jiji kubwa mno ulimwenguni na lililo asisisiwa miaka ya 1500+ lina hadi misitu au park (The Adirondack Park) njoo Dar kwa Frame economy ambako Nature haihitajiki kinacho hitajika ni Frame.
 
Jaribu kuwa una pitia ilani ya chama cha mapinduzi kuanzia Mwinyi, Mkapa, Jakaya, John na Tusubirie ya Mh Rais

Utapata angalau mwanga kwa maswali yako, au maswali yako yaende moja kwa moja kwenye Ilani ya chama tawala maana hao ndio wanatakiwa kuhojiwa.

Na ili uweze kuwa hoji ni lazima usome ilani yao.
 
Wakati wenzetu wakiwa na plan za miaka 100 ijayo Bongo tuna plan za wiki 5 zijazo. Nchi ina plani za kisiasa na ziko Surported na wajinga hili Taifa la Tanzania.

Tanzania kuna plan za wiki chache mbele, kila mara ni Bomoa hiki weka hiki, badili hiki weka hiki.

Mfano Chukulia ujenzi wa kituo cha Mabasi cha Ubungo wale wahuni walitarget miaka mingapi mbele? Angakia sasa kituo kisha kufa kimepewa majukumu mapya ambayo hayakuwepo kabisa.

Ile Mbezi kituo cha Mabasi baada ya miaka 7 kuanzia sasa itaonekana ni pafinyu sana,pako mjini sana katikati sana hivyo wanatafuta eneo jipya wahamishe stendi na pale wajenge hata soko la wamachinga, na sisi Wajinga tutashangilia sana mno.

Raisi anatwaaa aridhi Dar kisa ujenzi wa miundo mbinu ya mabasi yaendayo kasi, sasa jiulize Nchi nzima hakuna alie kuwa anawaza kitu kama hchi miaka 30 iliopita?

Tuombe uzima baada ya miaka kadhaa itaonekana tena hizo Barabara za mwendo kasi hazifai watavunja wajenga njia za treni za kuzunguka Dar na pia watatwaa aridhi.

Miji inajengwa kiholela sana, miji imejaaa frame, miji haina maeneeo ya akiba, miji imejaaa majengo tupu, miji ina plan za mwaka mmoja mmoja mbele.

Sijui nani alieawadanganya Watanganyika kwamba miji ni majengo yenye Frame, make miji imejaaa mno Frame hakuna space tena.

Fikiria jiji kama New york Jiji kubwa mno ulimwenguni na lililo asisisiwa miaka ya 1500+ lina hadi misitu au park (The Adirondack Park) njoo Dar kwa Frame economy ambako Nature haihitajiki kinacho hitajika ni Frame.
Wakati tunapata uhuru, Dar es Salaam ilikuwa na watu wasiozidi 200,000. Leo ina wakazi zaidi ya milioni 6. Projections zinasema idadi hiyo itaongezeka mpaka watu milioni 13 mwaka 2035, miaka 11 ijayo. Idadi hiyo ni zaidi ya population ya Tanganyika ya watu milioni 10 tulipopata uhuru.

Yote haya yanatokea bila ya kuwa na Masterplan yeyote ya maana. Maamuzi yanafanywa kisiasa kuliko kiweledi kwa kuangalia hali ya sasa na sio miaka 50 ijayo.

Mbaya zaidi ni kuwa miundombinu ni ile ile iliyoachwa na mkoloni na kuongezwa kidogo na Nyerere!

Uko sahihi Mkuu.

Amandla...
 
Hili eneo ni kama tumefeli kufikiri. Nchi yote ipo hovyo hovyo tu.
Nenda Arusha huko ndio utaona vichekesho. Ulegelege wa serikali na kuendekeza sio inatugharimu sana.

Dar inaenda kuongoza kuwa jiji linalokua kwa kasi afrika miaka michache ijayo. Same kwenye majiji mengine. Lakin hakuna plan za maana zinafanyika. Tunajiendea tu.
 
Utakuta eneo sio la ujenzi wa ghorofa ila unaenda katika halmashauri na unapewa kibali kwa mlango wa nyuma. Nyumba inapanda kama uyoga tena bila viwango. Hii ndio bongo.
 
Hamna kitu hapo.waulizeni mradi wa jangwani pale kujenga nyumba 14,000 umeishia wapi?na mkopo wa dola million 500 kachukua
 
Tusijekushangaa Dar nayo imeshauzwa kwa Mwarabu!
Maana hayo yote yanafanyika kinyemela bila wananchi kuhusishwa!
 
Back
Top Bottom