TANGAZO:Wizara ya viwanda na Biashara Yajito kudhamini kozi ya Vipimo na Mizani(BLM)

TANGAZO:Wizara ya viwanda na Biashara Yajito kudhamini kozi ya Vipimo na Mizani(BLM)

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,217
BLM(BACHELOR IN LEGAL INDUSTRIAL AND METROLOGY).

Chuo cha biashara na uchumi,jana kimetoa tamko kupitia Mkurugenzi wake wa Mafunzo Dr Nangiwa kuwa Wamepokea taarifa kutoka Wizarani,imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Bi ADIJA kuwa wizara haitakuwa na fedha za kuwadhamini wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kozi hiyo ambayo hutolewa na CBE TU tena tawi la Dar es salaam.
Akizungumza kwa umakini kabisa Dr Nangiwa kwamba yeye amepokea Maelekezo hayo kutoka Kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Ahmed Ahmed kuwa sasa wanafunzi watatakiwa kujitegemea kulipa ada ambayo ni 1232000 kwa mwaka.

Ikumbukwe kuwa taarifa hizi zimetoka huku wanafunzi wakiwa teali wamesha sajiliwa na Chuo.kutokana na sintofahamu hiyo Chuo kimeamua kufuta Usajili kwa Wote waliosajiliwa tareh 15 oct 2012 bila kulipa chochote na kutakiwa kulipa ili wapate usajili upya.

Angalizo.
Mwaka wa 3 wapo wanafunzi 18, ndani ya hao wengi wao ni watumishi wa wizara tofauti.wote wanadhaminiwa na Wizara.

Mwaka 2 wapo 37,wote wanadhaminiwa na wizara.

Mwaka wa 1 wapo 25 ambao kati yao hawana sifa ya kusoma kozi hyo.
Ili usome kozi hyo ni lazima uwe Umesoma Technical college,PCM AND PGM.Lakini wapo waliopata nafasi kusoma kozi hiyo wakiwa wamesoma HGE,EGM NA PCB.
 
Kama wana sifa waende wakakope Bodi ya Mikopo
 
Back
Top Bottom