Tangu apatwe na stroke, ni miezi saba sasa hawezi kutembea. Msaada wa kitaalam tafadhali

Tangu apatwe na stroke, ni miezi saba sasa hawezi kutembea. Msaada wa kitaalam tafadhali

Hii kitu ni chronic case ndugu yangu. Mpeleke Muhimbili for CT scan ili wataalamu wajitanue ktk kumtibu Mzee!
 
Haya yote unayajua kwa kufanya CT-Scan japo unaweza kukisia kwa kutumia historia ya mgonjwa e.g historia ya BP inaweza kukupa clue!
Kwa maelezo haya yamenifanya nigoogle types of stroke nimegundua 87% ya stroke ni ya Ischemic(clots). Umesema unaweza kugundua pia kwa historia ya mgonjwa na hapa nakumbuka kauli ya Dr. flani nilimhoji kuhusu recovery ya mzee. Alisema wapo ambao wanarecover within a short time, wengine they don't recover kabisa kulingana na aina ya stroke, akanambia sifikirii kuwa stroke ya mzee ni hemorrhagic (nadhani hii ni mbaya kuliko). Sasa mkuu nisaidie hapo pa KUKISIA KUTOKANA NA HISTORIA YA MGONJWA.
 
Watu wenye tatizo la Pressure kuwa juu mara nyingi hupata Hemorrhagic stroke nje na hilo pale anapopata stroke sababu damu inavujia kwenye Ubongo...Basi kuna Pressure inaongezeka ndani ya ubongo(Chukulia Fuvu la kichwa linabeba kilo tano za Ubongo afu ghafla zinaongezeka gram 100 za Mabonge ya damu) hivo mgonjwa kichwa kitamuuma na atakua anatapika!
^
Mgonjwa akija na hivo vitu vitatu | BP, Vomiting na Headache cha kwanza kuwaza ni damu kuvilia kwenye Ubongo!

Kumbuka hii haimaanishi mtu mwenye BP ilo juu hawezi pata Ischemic stroke ndo maana kuacha kubahatisha na kutumia sayansi za dalili inatubidi mwisho kufanya CT scan kama Confirmatory hii pia inatusaidia kujua Extent ya damage!

Na kama Ni ischemic stroke/ Clots kuna dawa ya kulainisha damu isije ganda na stroke kujirudia ndo maana jana nkakuuliza baadhi ya maswali ya dawa anazotumia ili nijue kama dawa ya namna hii ipo....Kumbuka usijaribu kumpa mgonjwa dawa za hivo kama haujafanya CT scan maana kama ana Hemorrhagic sttoke damu itavilia zaidi kwemye Ubongo!

Nje na hizo dalili kuna kitu kingine kinaitwa Subarachnoid Hemorrhage tunaweza kifananisha na Hemorrhagic stroke lakini tofauti ni wapi damu inavilia.
Hii nayo approach yake ni tofauti katika matibabu!

Sijaribu kukujaza na maneno ya kitabibu ila najaribu kukuonesha Umuhimu wa CT scan unavobadirisha matibabu ya wagonjwa walopooza!

Kwa Hospitali za Serikali( Muhimbili na Mlonganzila ) ni kama 150,000/= kama una barua ya rufaa!

Kama pesa ipo jitose!
Kwa maelezo haya yamenifanya nigoogle types of stroke nimegundua 87% ya stroke ni ya Ischemic(clots). Umesema unaweza kugundua pia kwa historia ya mgonjwa na hapa nakumbuka kauli ya Dr. flani nilimhoji kuhusu recovery ya mzee. Alisema wapo ambao wanarecover within a short time, wengine they don't recover kabisa kulingana na aina ya stroke, akanambia sifikirii kuwa stroke ya mzee ni hemorrhagic (nadhani hii ni mbaya kuliko). Sasa mkuu nisaidie hapo pa KUKISIA KUTOKANA NA HISTORIA YA MGONJWA.
 
Mkuu pole kwa matatizo ila kwa uzoefu Wang km kuna daktar was tiba mbadala mpeleke kwasababu uko hospital utapigwa hela na tatzo lisipoe
 
Asante kwa majibu mazuri mkuu
Mzee hatumii dawa nyingine nje ya zile za BP akina Captopril, bendro na zingine. Labda kama ana kesi mpya ikiripotiwa kwa dokta siku za clinic anaweza pewa za maumivu nk. Zipo za kuchua ambazo huwa tunanunua toka kwa wataalamu kama dawa za kisuna etc. Pia CT scan hajawahii fanyiwa. Hivyo hatujui kama anatatizo jingine zaidi ya hili la sasa.
Alitibiwa hospital gani bila CT scan?
Mimi nilipata stroke Mwaka 2010 sikuwa na historia ya pressure. Kwa sasa nimerecover japo siyo 100% ila najitegemea kwa kila kitul
 
Alifanya CT scan?
Nje ya dawa za pressure anatumia dawa nyingine?
Hana tatizo jingine la moyo nje ya Hypertension?

Nachojaribu kuuliza anatibiwa kama mgonjwa wa damu ilovilia kwenye ubongo au anatibiwa kama mgonjwa wa ubongo ulokosa Oxygen?

All in All kikubwa katika stroke nikuhakikisha mgonjwa anafanya Physiotherapy,Kama yuko bedridden ni kuhakikisha mnamgeuza geuza asijepata Pressure sores ambazo zitafanya watu wam neglect.
Hakikisha anazingatia matibabu maana unaweza pata Second Stroke.

Kikubwa zaidi kinachowaua hao watu wa stroke ni Kupaliwa chakula hivo kuweni makini anapolishwa.

Unaweza angaika sijui kutumia madawa ya kienyeji na Blah Blah nyingi ila ukielewa sayansi juu ya ugonjwa huo hautathubutu hata kupoteza mda na hizo dawa za kienyeji ambazo nyingi ni za kubahatisha!

Tunaweza kutembea kunyosha mikono sababu kuna Sehemu ya Ubongo inatu control kufanya hivo...Kwa wagonjwa wa Stroke sehemu hizo zinakua zimekufa kwa kukosa oxygen au kwa kuvilia damu eneo hilo!
Recovery itategemea na extent ya cells za ubongo zilizokufa na kama zimekufa zimekufa tu...Hamna Reversal!

Principle ya Stroke ndani ya mwaka mmoja ni kwamba

1)Theluthi Moja watakufa
2)Theluthi nyingine wanakua vilema na wanaitaji msaada/Tegemezi
3)Theluthi ya mwisho wanaweza ku regain na kuwa wakujitegemea kwa kila kitu.

Endelea kukazania matibabu ya hospitali ili mzee awe kwenye hiyo theluthi ya #3.

Na kawe ambassador kwa wale wagonjwa wa pressure wanaokutwa na Pressure wakafanya mzaa na matibabu ya Hospitali ya kumeza dawa mpaka umauti wao maana siku yaja!

Mwisho kabisa ujibu maswali yangu mawili nilokuuliza mwanzo wa post hii ili nipate kuongeza nyongeza yangu ambayo itamsaidia mzee katika recovery!

Kama brain cells “zikifa zimekufa tu” akizingatia madawa ya hospitali “ili aingie kundi #3” itasaidia?

Nimeanza kuelewa kwa nini watu huwa wanalazimika kwenda kutafuta matibabu nje, as cripplingly expensive as it is. Maelezo ya madaktari wetu huwa ni hafifu hafifu tu yanakuacha njia panda.

“Kikubwa cha kuzingatia ni physiotherapy... kikubwa zaidi kinachowaua ni kupaliwa... Hakikisha unazingatia matibabu maana unaweza kupata second stroke... kama brain cells zimekufa zimekufa tu”!

Kwa hiyo hao wanaokufa, 1/3 ya wagonjwa, wanakufa kwa kupaliwa na chakula! Basi huu sio ugonjwa hatari kihivyo!
 
Jamaa amenpa mwanga sana, amenijuza mengi sana siyo mtu wa kumbeza. Ametumia muda wake mwingi mkuu kunielewesha.
 
Alitibiwa hospital gani bila CT scan?
Mimi nilipata stroke Mwaka 2010 sikuwa na historia ya pressure. Kwa sasa nimerecover japo siyo 100% ila najitegemea kwa kila kitul
Uliparalaizi?
 
Kwa kaji elimu kwangu kadogo chumba anacholala mzee hakikisha kina hewa ya kutosha.
Ikiwezekana nunua BP monitor na diary na urekodi kila siku mzee anapoamka, mchana na jioni na uende na vipimo kwa daktari siku ya clinic
Kama unaweza kumpata physiotherapist she amfanyie mzee mazoezi nyumbani na nyinyi mkiangalia.

2nd strike huwa ni mbaya sana jaribuni kuizuia
 
Jamaa amenpa mwanga sana, amenijuza mengi sana siyo mtu wa kumbeza. Ametumia muda wake mwingi mkuu kunielewesha.

Ukweli na mwanga unaotolewa na maelezo hautegemeani na ametumia muda gani kutoa maelezo.

Amemkatisha tamaa mgonjwa kwa kusema kama brain cell zimekufa zimekufa tu! Sasa azingatie dawa dawa gani?

Halafu anasema for the most part kinachomuua mgonjwa wa kiharusi ni kupaliwa chakula. Stroke hatari yake inakuua kwa kupaliwa! Most epically ridiculous medical commentary in the history of pathology, this guy is a quack, daktari wa mikorogo ya kimasai.
 
Stroke zipo aina mbili
Unaweza kupata stroke kwa kutokana na maradhi mbali mbali ikiwemo moyo,presha,stress na hata sukari nk,

Stroke aina ya pili ni ya kulogwa au kuingiwa na jini

Stroke ya maradhi mbali mbali
Pima presha tujue ni shinikizo la juu au chini na kipimo kinasemaje ;

Pima sukari tujue mzee anasukari ngapi?

Pima moyo vipimo vya ,
CT SCAN
MRI
ECHO
ECG

PIMA damu
HB
damu yake ni nzito au nyepesi
damu yake aina fangas

Pima cholestrolor

Swali je ,mzee wako ukiondoa hiyo presha anatatizo gani jingine
Labda uwa kuna vitu gani anavisikia kwenye mwili wake labda ganzi,miguu kuwaka moto,kichwa kuuma,kifua kuuuma,kusikia usingizi mara kwa mara
Funguka,,

Sisi wengine tulipata hayo matatizo
Tulicheza miguu yote miwili
Lakini ni baada ya vipimo kupima

Pili zingatia vyakula
Asile chakula chenye mafuta
Asile chumvi nyingi
Anywe maji mengi

Mimi ni kijana niliacha srarehe zote mara moja
Pombe
Mademu
Sigara
Mirungi

Nikawa nafanya mazoezi ya kutembea kwa miguu kwa speed kali
Asubuhi na jioni
Japo nilikuwa nayumba sana na kusikia kizungu zungu mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom